Rais
Jakaya Kikwete akitawazwa kuwa Omukama (Chifu) wa Missenyi wakati wa
ziara yake ya siku sita mkoani Kagera. Anayemsimika ni kiongozi wa wazee
wa Missenyi, Mzee Ernest Babeiya.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara
ya Kyaka-Bugene kwa kiwango cha lami katika kijiji cha Bunazi, mkoani
Kagera, akiwa na mawaziri alioongozana nao katika ziara yake hiyo ya
siku sita mkoani humo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari wa
vyombo mbalimbali wa mkoa wa Kagera ambao waliongozana naye katika ziara
yake ya siku sita mkoani humo. Rais Kikwete amewapongeza wanahabari hao
na kutoa shukurani nyingi kwa kazi nzuri ya kuufahamisha umma kila
hatua ya ziara yake kwa ufasaha na weledi.
Wanahabari hao pia
wamefurahi kuona kwamba Rais hakuja na jopo la wanahabari kutoka Dar es
salaam kwa kuwaamini wao, hatua anbayo wamesema imewapa faraja na
furaha kubwa na kujiamini zaidi.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuzindua rasmi ujenzi wa
barabara ya Kyaka-Bugene kwa kiwango cha lami katika kijiji cha Bunazi,
mkoani Kagera, akiwa na mawaziri alioongozana nao katika ziara yake
hiyo ya siku sita mkoani humo.
إرسال تعليق