WANAMICHEZO 102 kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) watashiriki katika
michezo ya majeshi kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo itafanyika
Nairobi, Kenya kuanzia tarehe Jumatatu Agosti 5, 2013 hadi Agosti 17, 2013.
Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania alitarajiwa kukabidhi Bendera ya Taifa kwa
wanamichezo hao mchana huu tukio ambalo lilitarajiwa kufanyika bwalo
la askari katika kambi ya Twalipo Administration Unit (TAU) iliyopo
mkabala na Chuo cha Uhasibu, Dar es
salaam.
Vyombo
vya Habari vinakaribishwa kuchukua matukio katika hafla hiyo ya makabidhiano.
Kwa mawasiliano zaidi tel no_0715 270 236,
0754 270 236
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP 9203
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk
إرسال تعليق