Ofisi zaidi ya 12 za mabalozi wa Marekani katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini zimefungwa. Hatua
hiyo inafuatia serikali ya Marekani kusema Ijumaa kwamba inaamini kuwa
al-Qaeda au kundi linaloshirikiana na al-Qaeda huenda likawa linapanga
mashambulio.
Ubalozi wa Marekani mjini Kabul piya umefungwa kwa sababu ya ilani hiyo kuhusu usalama.
Mataifa
kadha ya Ulaya nayo yamefuata - Uingereza, Ufaransa na Ujerumani
zimesema kuwa balozi zao mjini Sanaa, Yemen, zitafungwa mwisho wa juma.
Chanzo - BBC Swahili
إرسال تعليق