Barcelona wafanya mauaji kwa Santos ya Neymar yawapiga goli 8 - 0

Masupastaa: Lionel Messi na Neymar wakifurahi kabla ya mechi



 Ndo mwanzo wa mataji? Barca baada ya kutwaa kombe la Joan Gampar

BARCELONA imeiangushia kipigo kizito cha 8-0 Santos ya Brazil kwenye uwanja wa Nou Camp na kutwaa taji la Joan Gamper katika mwendelezo wa mechi za maandalizi ya msimu mpya.

Neymar aliyesajiliwa kwa pauni 48 alianzia benchi dhidi ya timu yake ya zamani sambamba na mchezaji anayewaniwa na Manchester United Cesc Fabregas ingawa kiungo huyo wa zamani wa Arsenal alifunga mabao mawili katika kipindi cha pili.

Alexis Sanchez, Pedro na Lionel Messi kila mmoja alifunga bao moja katika kipindi cha kwanza, wakati bao la kujifunga mwenyewe la Leo na magoli mengine kutoka kwa Adriano, Jean Marie na mawili ya Fabregas yalihitimisha karamu hiyo ya magoli.

Supastaa wa samba Neymar ambaye alicheza mchezo wake wa kwanza kwenye jezi ya Barcelona katika mchezo wa sare ya 2-2 huko Poland, alionekana akitaniana na mchezaji bora wa dunia Messi kabla ya kucheza mechi yake ya kwanza mbele ya mashabiki wa Barcelona kwenye uwanja wa Nou Camp.

Messi alikuwa wa kwanza kufunga katika dakika ya 8 na muda mfupi baadae krosi ya nguvu ya Dani Alves ikamlazimisha beki Leo kujifunga.

Uchawi wa Messi ukahamia kwenye kusaidia kufunga mabao baada kumtengenezea winga wa Chile, Sanchez aliyekwamisha wavuni bao la tatu kabla ya Pedro kumalizia pasi ya Jordi Alba na kuhesabu goli la nne.

Kuingia kwa Neymar kulipokewa kwa shangwe kubwa kutoka kwa mashabiki waliojazana Nou Camp ingawa mtu mmoja aliyevalia nguo zenye nembo ya timu pinzani ya Santos, Internacional alivamia uwanja huku akimfuata Neymar kabla hajazuiliwa na kuondolewa uwanjani.

Vurugu: Neymar akiokolewa dhidi ya shabili mwenye hasira
 Maelekezo: Kocha mpya Tata Martino (kulia) akimpa maelekezo Neyma
Magoli yake ya mwisho? Fabregas alitokea benchi na kufunga mabao mawili

Post a Comment

أحدث أقدم