Shirika
la habari la Uingereza BBC limeomba radhi kwa kile wanachodai kuwa
walionesha kwa bahati mbaya video yenye picha ya Prince William wa
Uingereza ikiwa imechorwa nyeti za mwanaume katika uso wake.
Inadaiwa kuwa siku ya Alhamisi asubuhi (August 1) kituo cha TV cha
BBC kilirusha video ya wimbo “I Could Have Married Kate” ya kikundi cha
muziki cha Comedy kiitwacho ‘Barbershopera’ bila wao kugundua katika
video hiyo kuna picha inayomdhalilisha Prince William iliyochorwa nyeti
za mwanaume katika uso wake.
Watazamaji ndio waligundua picha hiyo na kuanza kutweet kuhusiana na walichokiona.
Baadae BBC waliomba radhi kwa kusema ‘Barbershopera’ waliwaletea
video hiyo na kwa bahati mbaya maproducer wao hawakugundua kasoro hizo
mapema.
“the material was provided by Barbershopera but we failed to spot the
offending material within it. We apologize for this.” BBC waliomba
radhi mchana wa siku hiyo.
إرسال تعليق