Bei za Nguo Juu Zanzibar.
Na Hafsa Golo
WAKATI wananchi wakijiandaa kwa sherehe ya sikukuu ya Eid el Fitri, bei za nguo zimepanda maradufu katika maduka mbali mbali yaliyopo Darajani mjini Zanzibar.
WAKATI wananchi wakijiandaa kwa sherehe ya sikukuu ya Eid el Fitri, bei za nguo zimepanda maradufu katika maduka mbali mbali yaliyopo Darajani mjini Zanzibar.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umegundua kwamba,
bei za nguo za kike za watoto zinauzwa kati ya shilingi 45,000 na 70,000
na nguo za watoto wa kiume zinauzwa kati ya shilingi 25,000 hadi
40,000.
Bei ya chini ya nguo za kiume ni kati ya shilingi 10,000 na 15,000 na
zinazouzwa bei hiyo ni zile zilizoganda madukani kwa muda mrefu na
kuonekana hazina hadhi tena.
Aidha viatu vya kitoto vinauzwa kati ya shilingi 20,000 na 35,000 katika maduka yaliyofanyiwa uchunguzi.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi, wafanyabiashara wamedai kwamba hali hiyo inatokana na ushuru kupandishwa.
Mmoja wa mfanyabiashara Abdurahman Ali ambae anauza nguo za kiume
alisema pamoja na ushuru mkubwa lakini pia sababu nyengine ni kushuka
kwa thamani ya shilingi ya Tanzania mbele ya dola.
Naye mfanyabiashara wa nguo za kike ambae hakupenda jina lake
liandikwe gazetini alisema mzigo alioingiza kipindi kilichopita alitumia
shilingi milioni nane lakini hivi sasa gharama imezidi mara mbili hivyo
haiwezekani kupunguza bei.
Hata hivyo, licha ya bei kuwa juu wananchi wamekuwa wakijazana katika vinjia vya mji wa Darajani kuwanunulia nguo watoto wao.
Zanzinews
إرسال تعليق