Mtoto
Ashura Mustapha (7) mkazi wa Mwandege, wilayani Mkuranga, Pwani
anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi tangu akiwa na mwaka mmoja.
Akizungumza
na mwandishi wetu, baba mzazi wa mtoto huyo, Mustapha Makombe alisema:
“Mwanangu anateseka sana jamani, ugonjwa ulianza kama malengelenge akiwa
na umri wa mwaka mmoja tukawa tunakwenda hospitali ndogondogo lakini
baadaye tukaamua kumpeleka Muhimbili ambapo tulipewa barua ya
kutuelekeza kwenda CCBRT, kule ndipo wakagundua mwanangu ana kansa ya
ngozi steji ya nne.
“Baada
ya kuhangaika katika hospitali nyingi bila mafanikio, nikaamua kwenda
Hospitali ya Regency (Dar) kuomba msaada wa kwenda kutibiwa India.
“Pale
waliniambia nichangie shilingi milioni moja na laki tano kwa ajili ya
tiketi na viza ili mwanangu akatibiwe India, hizo hela mimi sina. Naomba
Watanzania mnisaidie hata kwa fedha za mitandao kwa namba 0769 517765
ili niweze kumpeleka mwanangu India akatibiwe,” alisema baba mzazi.
Post a Comment