Baada
ya Nicki Minaj, Mariah Carey na Randy Jackson kuthibitisha kutoendelea
na msimu ujao wa shindano la kusaka vipaji ‘American Idol’ msimu ujao,
kuna dalili za Jeniffer Lopez kurejea katika meza ya ujaji wa shindano
hilo mwakani.
Chanzo kimoja kimeiambia Peoples Magazine kuwa J Lo yuko
katika hatua za mwisho za kusaini mkataba na American Idol kwaajili ya
kuwa jaji katika msimu wa 13 wa shindano hilo linalotegemewa kufanyika
mwakani.
J-Lo mwenye miaka 44 alikuwa jaji katika misimu miwili mfululizo
kabla ya kujiengua mwaka jana kwasababu alihitaji kupata muda zaidi wa
kufanya maswala yake ya muziki ikiwa ni pamoja na world tour.
Kwa mujibu wa Entertainment Weekly mastaa wengine ambao inasemekana
kuna uwezekano mkubwa wakawa katika panel ya majaji wa Ameican Idol
msimu ujao ni pamoja na Keith Urban, Jennifer Hudson na producer na
mwimbaji wa Black Eyed Peas Will i.am.
Msimu wa 13 wa American Idol kwa sasa upo katika pre production na unategemewa kuzinduliwa January 2014.
إرسال تعليق