Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,
Mhe. Angela Kairuki (katikati-mstari wa kwanza) akifuatana na Balozi wa
Vietnam alimaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Nguyen Duy Thien
(kulia), Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Mhe.
Balozi Juma Khalfan Mpango (kushoto mstari wa nyuma), Mkurugenzi wa
Idara ya Diaspora, Balozi Bertha Semu-Somi na Mkurugenzi Msaidizi, Idara
ya Asia na Australasia, Bw. Omar Mjenga walipokuwa wanawasili katika
Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro kwa ajili ya hafla fupi ya kumuaga
Balozi Thien.
Mhe. Kairuki akizungumza kuhusu
uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Vietnam wakati wa hafla hiyo
huku Balozi Thien na Mkewe wakimsikiliza.
Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi
zao hapa nchini Balozi Mpango nae akizungumza machache wakati wa hafla
hiyo huku Mhe. Kairuki, Balozi Thien na wageni wengine waalikwa
wakimsikiliza.
Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Asia na
Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Bw. Omar Mjenga akiwakaribisha wageni waalikwa kwenye hafla ya kumuaga
Balozi Thien ambaye amemaliza muda wa kazi hapa nchini. Wengine katika
picha ni Balozi Mpango na Balozi Semu-Somi.
Mhe. Kairuki akimkabidhi Balozi Thien
na Mkewe zawadi ya picha ya kuchora ya Mji Mkongwe wa Zanzibar kama
kumbukumbu yao kwa Tanzania.
Mhe. Balozi Nguyen Duy Thien na Mkewe wakimsikiliza Bw. Mjenga (hayupo pichani).
Picha na Reginald Philip.
إرسال تعليق