Nchini Uingereza Mama na Baba wa
kambo wa mvulana wa miaka minne aliyekufa njaa baada ya kufungiwa ndani
ya chumba kimoja kwa miezi minne wamefungwa maisha jela kwa makosa ya
kumuua mwanao.
Jaji aliyetoa hukumu hio amesema. Magdelena
WOO-TCHAK na Marius KREZ-OH-WEK wanastahili kutumikia kifungo cha miaka
39 gerezani kabla ya kupatiwa nafasi ya kukata rufaa.Wakati wa kesi hio daktari mmoja alisema mwili wa mtoto Daniel Pelka ulifanana na waathiriwa wanaofungiwa kwa jela bila chakula.
Kumekua na shutuma za umma kutaka kujua sababu za mtoto huyo kutookolewa licha ya mwili wake kupatikana na majeraha.
Wakati mmoja mtoto huyo alionekana akitafuta chakula kutoka kwa majaa ya taka. Wakati alipokufa mtoto huyo alikua na uzani wa kilo 10 ambao huwa ni uzani wa mtoto mchanga wa mwaka mmoja.
إرسال تعليق