Njia Panda; Moses Oloya amesema hajajua atabaki Vietnam, au atakuja Simba au Yanga |
Na Frank Sanga,
MCHEZAJI wa Xi Mang Saigon ya Vietnam, Moses Oloya amekiri kupokea tiketi ya ndege aliyotumiwa na Yanga, lakini akasema hajachagua timu ya kuichezea kati ya Simba na Yanga.
Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Vietnam jana Ijumaa, mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uganda alisema amefanya mazungumzo na klabu zote mbili; Simba na Yanga lakini atafanya uamuzi wa mwisho Agosti 31 baada ya mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Vietnam.
“Mkataba wangu unakwisha mwishoni mwa Oktoba, lakini mechi za Ligi Kuu Vietnam tunamaliza Agosti 31,” alisema.
Haya ndiyo mahojiano ya Mwanaspoti na Oloya yaliyofanyika jana Ijumaa saa 9:15 alasiri kwa dakika 12.
Mwanaspoti: Kuna utata hapa Tanzania, ni timu gani unakuja kuichezea msimu ujao?
Oloya: Ngoja nikuambie ukweli, mpaka sasa sijaamua kati ya Simba na Yanga.
Mwanaspoti: Kwani umefanya mazungumzo na timu zote mbili?
Oloya: Ndiyo karibu kila siku ninazungumza na watu wa Simba na Yanga.
Mwanaspoti: Umewaambia nini?
Oloya: Nimewaambia wasubiri nimalizane na timu yangu ya Saigon.
Mwanaspoti: Utamalizana lini na timu yako ya Saigon?
Oloya: Tutamaliza mechi ya mwisho ya ligi Agosti 31, lakini mkataba wangu unakwisha Oktoba mwishoni
Mwanaspoti: Mbona tunasikia upo Dar es Salaam?
Oloya: Hapana, nipo Vietnam.
Mwanaspoti: Kwa mara ya mwisho umekuja lini Dar es Salaam?
Oloya: Kwa mara ya mwisho nimekuja Dar es Salaam Kombe la Chalenji mwaka jana.
Mwanaspoti: Mbona tunasikia umekuja Dar es Salaam wiki hii?
Oloya: Hapana, nipo Vietnam, tena nipo na Geoffrey Kizito hapa tunakwenda kupata chakula cha jioni (Namsalimu Kizito).
Mwanaspoti: Lakini moyoni unaijua timu utakayochezea msimu ujao?
Oloya: Zipo timu tatu, timu yangu (Saigon) bado wapo fifte fifte, halafu kuna hizo Simba na Yanga. Bado sijajua timu ambayo nitaichezea. Itategemeana na makubaliano.
Mwanaspoti: Mbona tumeambiwa Yanga wamekutumia tiketi ya ndege?
Oloya: Ni kweli, Yanga walinitumia tiketi ya ndege, ambayo ilitakiwa niwe Dar es Salaam Alhamisi na kurudi Ijumaa wiki hii.
Mwanaspoti: Mbona umeshindwa kuja Dar wakati tayari ulitumiwa tiketi na Yanga?
Oloya: Klabu yangu imekataa kuniruhusu, kwa sababu tuna mechi muhimu kesho (leo Jumamosi) dhidi ya Da Nang.
Mwanaspoti: Hiyo tiketi ilikuwa ni ya ndege gani?
Oloya: Qatar Airways
Mwanaspoti: Kwa hiyo ulitaka kuja kusaini mkataba Yanga?
Oloya: Nilitaka kuja kuwasikiliza.
Mwanaspoti: Kwa hiyo mpango wako ni upi kwa Yanga na Simba?
Oloya: Wameniambia nimalizane na klabu yangu (Saigon) na hicho ndicho ninachokifanya, ingawa pia timu yangu bado haijawa wazi kama itanipa mkataba mpya au la.
Maelezo ya ziada
Baada ya mechi ya leo Jumamosi, Saigon itakuwa imebakiza mechi nne dhidi ya Kien Giang, Song Lam Nghe An, Hoang Anh Gia Lai na Long An.
Saigon inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 23 katika msimamo wa Ligi Kuu Vietnam yenye timu 12.
Usajili wa awali wa Ligi Kuu Bara msimu ujao unafungwa Jumatatu saa 6.00 usiku lakini utafungulia tena kwa muda wa wiki mbili kuanzia Agosti 15 na kwamba hadi jana Ijumaa jioni Simba na Yanga zilikuwa na wachezaji wanne wa kigeni kila moja na wanamsubiri mchezaji huyo kujazia orodha yao.
(Habari ni haki ya gazeti la Mwanaspoti)

Karibu Tanzania; Oloya kulia akiwa na mchezaji wa Azam FC, Mganda mwenzake, Brian Umony |

إرسال تعليق