JUMLA ya
warembo 15 kutoka katika vitongoji vine vya wilaya ya Ilala, wameanza mazoezi
ya kumsaka mrembo wa wa wialaya ya Ilala ‘Redd’s Miss Ilala 2013’ yanayofanyika
katika ukumbi wa klabu Billicanas uliopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Sindano
hilo litafanyika katika ukumbi wa Golden Jubilee Tower tarehe 16 Agosti mwaka
huu, kati ya hao warembo watatu ndio wanaowania nafasi ya kushiriki shindano la
Redds Miss Tanzania, shindano linalotarajia kufanyika baadae mwezi Septemba.
Warembo
hao ambao wanatoka katika vitongoji vya Mzizima, Tabata, Ukonga na Dar City
Centre wamekuwa wakijifua na kufanya onesho hilo kuwa la kuvutia zaidi, tofauti
na miaka iliyopita.
Maandalizi
ya shindano hilo yanaendelea vizuri na wamepania kuonesha vipaji vyao kwa
kufanya shindano la kuoesha vipaji ambalo linatarajiwa kufanyika wiki ijayo.
Sisi kama
kamati tunaowaomba wadau wa urembo kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia
muonekano mpya wa mashindano ya urembo, lakini pia kuoangalia jinsi Ilala
ilivyosheheni warembo watakaoleta ushindano mkubwa Redds Miss Tanzania 2013.
Warembo
waliopo katika kambi ya Miss Ilala ni pamoja na Alice Isaac, Clara Poul,Anna
Johnson,Iren Mwelolo, Munira Mabrouk,Rehema Mpanda, Shamim Mohamed, Martha
Gewe, Diana Joackim, Natasha Mohamed, Dorice Mollel, Pendo Lema, Kazumbe Mussa
na Kabula Kibogoti.
Hadi sasa
kampuni zilizojitokeza kudhamini ni Redd’s, Dodoma wine,CXC Tours,Chilly
Will,Tanzania Daima,Jambo Leo,Clouds FM,Tanzania Daima,City Lounge,Times FM na
Lemutuz Blog.
LE MUTUZ
Mratibu
إرسال تعليق