Meneja
wa mradi wa Tigo Kilimo Bw. Yaya Ndjore (kushoto) akiongea na
Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mkoani Dodoma kuelezea mikakati
walionayo kuwawezesha wakulima nchini kwa kujiunga na huduma hiyo ya
Tigo Kilimo ili kupata taarifa mbalimbali za kilimo ikiwemo mbinu bora
za kilimo, hali ya hewa na bei za mazao. Pembeni yake ni Meneja Biashara
wa Tigo mkoa wa Dodoma Bw. Saitoti Naikara.
Tigo
Tanzania imetoa rai kwa wakulima zaidi nchini kuchangamkia huduma ya
simu “Tigo Kilimo” kama namna ya kupata taarifa za kilimo ambazo
zitawawezesha kuzalisha zaidi na kupata taarifa bora za masoko kwa ajili
ya kuuza bidhaa zao kwa bei ya faida.
Akizungumza
na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa Tigo katika Sikukuu ya
Wakulima ‘Nane Nane’ itakayofanyika jijini Dodoma wiki ijayo, Meneja
Mradi wa Tigo Kilimo, Bw. Yaya Ndjore alisema kwamba tayari Tigo imetoa
teknolojia ya simu ya kisasa katika huduma ya kilimo ambayo inahusu
kifurushi maalum inayojumuisha namna bora ya kufanya kilimo, bei za
masoko kwa bidhaa za kilimo, pamoja na utabiri wa hali ya hewa.
“Toka
tuzindue huduma hii mwaka jana, kundi kubwa la wateja wetu kutoka kila
kona ya nchi wameweza kufaidika. Kwa maana hiyo tunapenda kuwaasa pia
wakulima wengi zaidi kujiunga na huduma hii ya Tigo Kilimo kwa ajili ya
kupata matokeo bora zaidi katika shughuli zao,” aliongeza Yaya.
“Tigo
inajivunia kuwa kampuni ya simu ya kwanza kutoa huduma za taarifa za
kilimo nchini Tanzania kupitia teknolojia ya simu za mkononi, ambayo
inaendana sambamba na utamaduni wetu wa ubunifu ambayo Tigo inapenda
kuonesha kila siku. Hakika majaribio ya teknolojia hii yamewapatia
mafanikio makubwa kwa wakulima ambao wamefaidi taarifa za uhakika kuhusu
mambo ya kilimo,” alisema Yaya.
Kutokana
na Yaya, Tigo inawahudumia wakulima kupitia meseji (SMS) kwa kutoa
taarifa za bei ya soko, utabiri wa hali ya hewa na namna bora ya
kuendesha kilimo kwa mazao yanaongoza kulimwa nchini kwa mfano mpunga,
mahindi, viazi mviringo na viazi vitamu, kwa kutaja machache.
“Wakulima
wana nafasi kubwa ya kufaidi huduma zetu si tu kwa sababu ya mtandao
wetu mpana wenye uwezo wa kumfikia kila mkulima nchini aliyejisajili,
bali pia kwa sababu mkulima hahitaji kulipia chochote kujisajili na
kuingia katika huduma hii, pamoja na hayo kupata muhtasari wa taarifa ni
bure pia,” aliongeza Yaya.
Kwa
kuongezea, wakulima pia wanaweza kupata huduma za vifurushi vya wiki
ambazo hazina kikomo katika idadi ya taarifa wanazoweza kupata, hii
inamwezesha mkulima kupata huduma hii bila vikwazo vyovyote.
Kuhakikisha
kwamba tunawapatia huduma bora wakulima katika mikoa yote nchini, Tigo
pia imeanza mkakati wa kuwa karibu na wateja wake kwa kuongeza ubora wa
minara na mtandao wake mikoani. Huduma hii ya “Tigo Kilimo” inapatikana
kwa kuingiza *148*14# katika simu aina yoyote ya mkononi yenye laini ya
simu ya Tigo.
إرسال تعليق