Idara
ya operesheni za ulinzi wa amani katika Umoja wa Mataifa imethibitisha
kuwa imefikia hatua ya mwisho katika harakati za kuagiza ndege
zinazoruka bila rubani kwa ajili ya kujaribiwa na ujumbe wa Umoja wa
Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO katika ulinzi
wa raia.
Ndege hizo zijulikanazo kama FALCO, zimeundwa kuwa na uwezo wa kuruka masafa ya wastani angani, na uwezo wa kubeba vidude vya aina mbali mbali vyenye uwezo wa kurekodi kinachoendelea katika maeneo wanakopaswa kulindwa raia.
Ndege hizo hazina silaha, na zinatarajiwa kupelekwa DRC katika wiki chache zijazo, ili kusaidia katika ulinzi wa raia dhidi ya makundi yenye silaha.
Ndege hizo zimeagizwa kutoka kwa kampuni moja ya Kiitalia, SELEX ES. Luteni Jenerali Paul Ignace Mella ni kamanda wa kikosi cha kulinda amani Darfur, UNAMID, na wakati wa mkutano wa makamanda wa vikosi vya kulinda amani hapa mjini New York, alitupa maelezo zaidi kuhusu ndege hizo:

Hizi ndege zisizo na rubani, zina uwezo wa kupiga picha, zikiwa angani, zikaona eneo lote, zikaona mienendo mbalimbali ya watu. Kwa hiyo kama kuna makundi yanayokwenda yanataka kuwadhuru raia, yanaweza yakaonekana mapema. Lakini siyo ndege tu, kuna rada pia, ground surveillance radar zina uwezo pia wa kuona. Kuna sensors mbalimbali kama vile cameras za kawaida na pia zina uwezo wa kupitisha zile taarifa kwa haraka. Mfano, hizo ndege au radar zikiona, saa iyo hiyo ambayo watu wako kambini wana uwezo wa kuona kwenye screen ni kitu gani kinachoendelea na wakachukua hatua papo hapo.
Taarifa ya Joseph Msami, Radio UM, New York
Post a Comment