HATARI: Wanafunzi watatu walawitiwa DAR... Yaleta hofu, watoto wahofi kwenda shule, Walimu wazidiwa kete
Wanafunzi
watatu katika shule ya msingi Majimatitu jijini Dar es Salaam,
`wamefanyiwa unyama wa kutisha’ baada ya kulawitiwa na kulazimishwa kula
mbegu za kiume.
Watoto
hao wenye umri wa miaka kati ya 9 na 10 (majina na madarasa yao
yamehifadhiwa), walifanyiwa vitendo hivyo kwa mwaka mmoja, mhusika
akidaiwa kuwa mkazi mmoja anayeishi jirani na shule hiyo.
Utafiti
wa gazeti hili ulibaini kuwa mtuhumiwa wa uovu huo aliyejulikana kwa
jina moja la Salum, alikuwa akifanya kitendo hicho ndani ya nyumba moja
ya vyumba viwili, jirani na shule hiyo.
Mtuhumiwa
huyo, anadaiwa kuwalipa watoto hao Shilingi 1,000 baada ya kuwalawiti
na kuwaamuru wamsafishe sehemu zake za siri kwa kumnyonya.
WATOTO WASIMULIA
Watoto
hao wameliambia NIPASHE Jumapili kuwa mtu huyo, alikuwa akiwafuata
shuleni na kuwachukua hadi katika nyumba hiyo na kuwaingilia.
Walidai kuwa, walifanyiwa kitendo hicho mara mbili, asubuhi wakati wakienda shule na mchana wakati wa mapumziko.
Kutokana na muda mwingi wanakuwa na mtu huyo, walishindwa kuhudhuria masomo darasani kama wanavyofanya watoto wenzao.
"Huwa
anakuja maeneo ya shule na kusimama nyuma ya mlingoti wa goli kwenye
kiwanja cha mpira wa miguu, kisha anatuita kwa ishara ili tumfuate,"
alidai mtoto mmoja.
Alieleza
kuwa baada ya kufika kwenye nyumba hiyo, watoto hao wanasimamishwa
kwenye varanda kabla ya kuitwa mmoja mmoja kuingia chumbani.
"Anapotuita
chumbani anatuambia tulale chini, anatulalia juu na kutulawiti,
tukisikia uchungu anatuziba mdomo tusilie halafu anatutishia kutuua
endapo tutamuambia mtu," alidai.
“anapomuingia
mtoto mmoja na kumaliza, anamlazimisha kumlamba na kula mbegu zake za
kiume kama njia ya kumsafisha ili aweze kumuita mtoto mwingine,”
ilielezwa.
Pia,
mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwa, akimaliza kuwalawiti, aliwapa chupa ya
maji safi waende kujisafisha kabla ya kuwaruhusu kuondoka.
ILIVYOGUNDULIKA
Siri
hiyo iligundulika baada ya mtoto mmoja kukutwa na wenzake akiwa na
Shilingi 1,000, alipotaka kumpatia mwenzake Shilingi 200 za kununua
mihogo.
Mariam
Kimata, ni mzazi wa mmoja wa watoto hao, alisema alibaini tukio hilo
kufuatia mwanafunzi mwenzake kwenda kumuuliza kama alimpa mtoto wake
fedha za matumizi shuleni.
"Yule
mtoto alikuja kwangu kuhoji kwa nini rafiki yake anakuwa na fedha nyingi
wakati huu wa Ramadhan, nilishtuka sana nilidhani mtoto wangu ameanza
tabia ya kuniibia," alisema.
Alisema, "kwa kawaida katika kipindi hiki baba yake hampatii fedha na kwa sababu amekuwa akitueleza amefunga."
Kimata,
alisema mtoto wake aliporudi kutoka shuleni alimuhoji jambo hilo, mwanzo
alikuwa akikataa na baadaye alikubali, lakini alisema aliokota njiani.
Hata hivyo, suala hilo lilifikishwa kwa baba wa mtoto huyo, ndipo alipoamua kusema ukweli kwa kuhofia kuchapwa voboko.
"Nilishtuka sana kiasi ambacho mapigo ya moyo yalishuka na kukimbizwa hospitali baada ya kusikia jambo hili baya," alisema.
HOSPITALI WATHIBITISHA
Kimata,
alisema mumewe alimchukua mtoto huyo hadi kituo cha Polisi cha Charambe
Majimatitu, kisha walipatiwa fomu ya PF3 kwa ajili ya kwenda hospitali
ya wilaya ya Temeke.
Alidai
kuwa daktari aliyemchunguza mtoto huyo alithibitisha kuingiliwa kinyume
na maumbile na kupelekea njia ya haja kubwa kuharibika.
USTAWI WA JAMII YAZUNGUMZA
Afisa wa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Temeke, Sharifa Ally, alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo dhidi ya watoto hao wawili.
Hata hivyo, watoto hao waliruhisiwa baada ya kufanyiwa vipimo pamoja na kupatiwa matibabu.
"Tumelipokea tukio hilo, lakini wenzetu Polisi wanaendelea kulichunguza ili mtuhumiwa aweze kukamatwa," alisema.
SHULE YAKIRI KUZIDIWA
Uongozi
wa Shule hiyo umejikuta katika hali tete baada ya kuzidiwa na vitendo
vya wanafunzi wake kulawitiwa na watu wazima au wanafunzi wenyewe kwa
wenyewe.
Mwalimu
Mkuu msaidizi, Abel Masawe, alisema kitendo walichofanyiwa wanafunzi
wake ni cha kinyama na kuiomba polisi kumkamata muhusika haraka.
Kwa
mujibu wa Mwalimu Masawe, matukio ya aina hiyo yameongezeka kwa kasi
shuleni hapo, kiasi ambacho inafikia watoto wenyewe wanafanyiana vitendo
hivyo wakiwa nje ya eneo la shule.
Naye Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke, Honorina Mumba, aliahidi kulishughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo.
Alisema kimsingi, mtuhumiwa lazima akamatwe kwa sababu amefanya kitendo cha kinyama kwa watoto hao.
MTUHUMIWA ASAKWA
Ingawa
polisi katika mkoa wa kipolisi wa Temeke haujatoa tamko kuhusu tukio
hilo, taarifa za uhakika zimeeleza kuwa jeshi hilo linaendelea kumsakata
mtuhumiwa wa uovu huo.
CHANZO: NIPASHE
إرسال تعليق