Msanii
mkongwe wa Hip Hop kutoka Morogoro, Afande Sele amesema amani ya
Tanzania ipo mikonini mwa Wanasiasa na Waandishi wa habari na kuwataka
Watanzania wawe makini kutokana na matukio ya uvunjifu wa amani ambayo
yamekuwa yakitokea.
Afande amesema kila Mtanzania anawajibu wa kuhakikisha amani iliyopo
inaendelea kulindwa na kuepuka Wanasiasa na Waandishi wa habari ambao
huchochea na kusababisha matukio ya uvunjifu wa amani.
“Swala la amani, ni haki ya kila mtu na kila mtu ana haki ya kulinda
amani kwahiyo tusiyumbishwe na wanasiasa na waandishi wa habari ambao
wamekuwa wakiwayumbisha Watanzania,wanasiasa wamekuwa wakiendesha
mikutano yao kwa maslahi yao. Kwa mfano swala kodi za “simcard”
wamejadili wabunge wetu kwani hawakutambua maisha ya Watanzania? Na
Wandishi wa habari wamekuwa wakiandika habari bila uchunguzi
wanasababisha machafuko,”
Aliendea kusema kuwa suala la ugumu wa maisha linasababishwa na
viongozi wetu wanaotambua maisha halisi ya Mtanzania mwenye kipato cha
chini.
“Maisha ya watanzania ni magumu,suala la simcard lilijadiliwa bungeni
na wakalipitisha wenyewe kwahiyo suala la ugumu wa maisha
linasababishwa na viongozi wetu.”
إرسال تعليق