Mali asisitiza kuanza maridhiano ya kitaifa

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita

Rais wa Mali amesema kwamba, mazungumzo ya maridhiano ya kitaifa kwa ajili ya kutatua migogoro ya maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo yataanza hivi karibuni. 

Ibrahim Boubacar Keita amesema hayo katika kikao cha kwanza na Baraza la Mawaziri na kusisitiza kuwa, ni jukumu la serikali kutatua kikamilifu migogoro ya maeneo ya kaskazini na kuimarisha amani ya muda mrefu chini ya msingi wa kuaminiana makabila tofauti ya nchi hiyo. 

Rais wa Mali Septemba 4 wakati alipoapishwa ili kuanza kuiongoza nchi hiyo pia alisema kwamba, miongoni mwa masuala yanayopewa kipaumbele na serikali yake ni kuanzisha mazungumzo ya maridhiano ya kitaifa.

Wakati huo huo Waziri mpya wa Madini wa Mali amesema kuwa serikali ya nchi hiyo itaangalia upya makubaliano ya madini na kuanza kuzungumza tena na mashirika ya kigeni kujadili mikataba ambayo haina maslahi na taifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post