Mwanamke Atengeneza Mimba Kuficha Dawa za Kulevya, Cocaine

RAIA mmoja wa nchi ya Canada amekamatwa nchini Colombia baada ya kujaribu kupanda ndege kurejea Canada akiwa na tumbo bandia la ujauzito alimokuwa ameficha dawa za kulevya aina ya Cocaine.
Mwanamke huyo aliyekuwa anajifanya kuwa mtalii akirejea Toronto, alihojiwa na polisi katika uwanja wa ndege wa Bogota aliyemshuku na kumuuliza alikuwa amesalia na miezi mingapi kujifungua.
Alijibu kwa ukali mno, hali iliyomfanya afisa huyo kumshuku sana na hivyo kumfanyia ukaguzi zaidi. Afisa huyo aligusa tumbo lake na kuhisi ilikuwa baridi mno na gumu sana ndipo askari hao wakaamua kumkagua zaidi.
walimkuta na dawa za kulevya zilizokuwa zimefungwa ndani ya tumbo bandia la mimba ambayo mwanamke huyo alikuwa amevaa kwa kufunga tumboni. Inasemekana kuwa alisema ana miezi saba ya ujauzito lakini baada ya polisi kumkagua walimpata na Cocaine kilo mbili iliyokuwa ndani ya vipochi viwili.
Mwanamke huyo atashtakiwa kwa kosa la ulanguzi wa madawa ya kulevya na huenda akafungwa jela kwa miaka mitano au nane. Mwaka huu pekee karibu watu 150 wamekamatwa na madawa ya kulevya katika uwanja wa ndege wa Bogota. Karibu thuluthi moja ya waliokamatwa walikuwa raia wa kigeni, kwa mujibu wa maafisa wakuu nchini Colombia.
-BBC

Post a Comment

Previous Post Next Post