MKUU WA MKOA WA PWANI AKEMEA TABIA YA WATENDAJI KUSABABISHA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA JAMII

Ben Komba, Pwani.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, BIBI.MWANTUMU MAHIZA amekemea tabia ya watendaji kusababisha migogoro ya ardhi katika jamii kutokana na utendaji wao kuongozwa na maslahi binafsi hali ambayo inatishia hali ya ulinzi na usalama nchini.
 
BIBI.MAHIZA amewaambia watendaji katika kikao cha kuhimiza maendeleo ya Mkoa wa Pwani kilichofanyika mjini Kibaha kuwa wanachoponzwa nacho ni tamaa ya vifedha vidogo vidogo wanavyopokea ndio kichocheo cha uvinjifu wa amani katika wilaya, Kata na Mitaa/vijiji.
 
BIBI.MAHIZA ameonya kuwa iwapo atabaini viongozi ndio wanahusika katika kuchonganisha raia, basi atahakikisha mhusika anachukuliwa hatua za kisheria bila kujali yeye ni chama gani au ni nani ili kuendeleza utamaduni wa kutii sheria bila shuruti.
 
Amewachukulia watu wanaowachonganisha wananchi katika masuala ni wabaya ambao wanasababisha uvinjifu wa amani.
 
Akiongea katika kikao hicho Mwenyekiti wa serikali Mkoani  A, BW.TITUS SAFIEL KABORA amesema kuna mambo ambayo jamii inayaibua lakini yamekuwa hayapewi kipaumbele, akitoa mfano kwa mtaa wake ambao umeibua barabara sugu tano ambazo walitaka zifunguliwe lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika.
 
BW.KABORA ameeleza kuhusu suala la ujenzi holela ambao umeibuka katika mtaa wa BLOCK B na kupewa nguvu na viongozi wa kisiasa na malalamiko yanapopelekwa hatua za nyingine, kuna kuwa hakuna majibu na kuacha sheria zikikiukwa.

Post a Comment

أحدث أقدم