PONGEZI ISSA MICHUZI BLOG KWA KUTIMIZA MIAKA TISA YA KUHABARISHA JAMII


SALAAM ZA PONGEZI KUTOKA HISIA ZA MWANANCHI


Tunatoa pongezi zetu za dhati kwa mwana habari mwenzetu ndugu Issa Michuzi na Blog yake 
www.issamichuzi.blogspot.com kwa kazi kubwa walioifanya na wanayoendelea kuifanya ya kuhabarisha jamii yetu kwa muda wa Miaka tisa (9) mfululizo bila kupumzika.

Blog ya Issa Michuzi imetimiza miaka 9 tangu kuanzishwa  tarehe 8 Septemba 2005 jijini Helsinki, Finland. 
Kwanza kabisa; tunampa hongera Ndugu  Michuzi kwa kuandika historia kwa kuleta mapinduzi ya habari ndani nchini na nje ya Tanzania.

Pili; tumefurahishwa sana kwa kitendo cha Ndugu Michuzi kurudisha shukrani na fadhila kwa Baba wa Ma-blog Bwana Ndesanjo Macha kwa kumtambulisha, kumuingiza na kumfungulia blog ya jamii ya  www.issamichuzi.blogspot.com mnamo tarehe 8 Septemba 2005 jijini Helsinki, Finland. 


Tatu; Pongezi za kipekee zimuendee Ndugu Issa Michuzi kwa kazi kubwa ya kutuhabarisha usiku na mchana pamoja na majukumu yake ya  kikazi akilitumikia vyema Taifa letu la Tanzania katika Ofisi Kuu kuliko zote akiwa kama  Mwanahabari Mpiga Picha (Photo Journalist) mwajiriwa wa Serikali akifanya kazi chini ya  Kurugenzi ya Mawasiliano, Ofisi ya Rais Ikulu ya Tanzania.

Nne; Ni ukweli usiopingika kwamba Issa Michuzi ni mtu wa watu, anapenda watu na ucheshi wake umemletea mafanikio makubwa katika tasnia ya habari. Kwa upande mwingine Michuzi ameitumia vyema nafasi ya kipekee aliyopata kutuhabarisha kwa kutujuza mambo mbalimbali yanayoendelea ndani na nje ya nchi. Hakuna ubishi tukijiuliza swali ni wafanyakazi wangapi waliopo sasa hivi Serikalini katika nafasi kama ya  Michuzi, ama waliopita ambao wamefanya mapinduzi ya habari kama Michuzi? 
Ndugu msomaji, ukweli unabaki palepale Michuzi anastahili pongezi za kipekee kwa kuthubutu.

Mwisho kwa kumalizia napenda kuufahamisha Umma kwamba  Bwana Issa Michuzi amekuwa mfano wa kuigwa na jitihada zake na mazingira yake kikazi yamekuwa chanzo cha mafanikio na umaarufu mkubwa aliojizolea na kujijengea jina nchini na nje ya nchi. Hongera kwa jitihada na harakati zako.
Tunatambua pia kwa nafasi uliyonayo kikazi inakupa mlango wa kupata habari kabla ya vyombo vingine vya habari kupata,  na vilevile kwa kuwa mwajiriwa wa Serikali umejijengea heshima kwa taasisi, wizara na vyombo vingine vya Kiserikali kukuleletea habari zao moja kwa moja wewe kwanza kabla ya vyombo vingine, kitu ambacho kimefanya watu wengi tuwe tunasoma blog yako na kuipenda kitu ambacho ni kuzuri na cha kuigwa.

Post a Comment

أحدث أقدم