Robo 3 ya mwaka: Wasanii 10 wa Bongo wenye moto zaidi

525ad02214c111e3831f22000a9f13a0_7
Diamond Platnumz
Tupo kwenye robo ya tatu ya mwaka 2013. Mwaka huu muziki wa Tanzania umeendelea kuonesha mapinduzi makubwa kuanzia uwepo wa show nyingi, malipo makubwa kwa wasanii, wasanii kuwekeza zaidi kwenye video nzuri na za gharama na thamani yao kuongezeka zaidi.
Ni wakati huu ambapo show za Serengeti Fiesta zinaendelea sambamba na Kili Music Tour. Kwa kuzingatia idadi ya show wanazofanya, nyimbo zao zinavyochezwa redioni, utambuzi wa kimataifa (international recognition) na namna wanavyopenya zaidi kimataifa hii ni list ya wasanii 10 walio hot zaidi mpaka wakati huu wa robo tatu ya mwaka.

Hakuna ubishi kwamba Diamond Platnumz ndiye msanii wa Tanzania aliye hot zaidi muda huu. Mwaka 2013 aliuanza vizuri mno licha ya kutokuwa na wimbo wowote mpya na rasmi zaidi ya Muziki Gani alioshirikishwa tu na Nay wa Mitego, Kesho uliotoka mwaka jana na Ukimwona na Mapenzi Basi ambazo si nyimbo alizoziachia rasmi, Diamond ameendelea kusikika kila kona ya nchini na kwingine na nyimbo zake zikipata rotation ya kutosha kwenye radio zote, kubwa na ndogo. Mwaka huu ameongoza kwa kufanya show nyingi kubwa ndani na nje ya nchi.
Kwa makadirio ya haraka, show alizofanya kuanzia Burundi na Congo, Kenya, Comoro na zile za Tanzania, tangu mwaka uanze hakuna shaka msanii huyo ambaye Bongo5 imempa jina ‘Bongo Flava Prince’ ameshaweka benki si chini ya shilingi milioni 500.
Siku chache zilizopita, ameongeza zaidi kasi yake kwa kuachia video kali ya wimbo wake Number 1, huku akitambulisha mtindo mpya wa uchezaji alioupa jina ‘Ngololo’. Kwa spidi aliyonayo, itachukua muda mrefu sana, Diamond kupokonywa kijiti chake cha nafasi ya kwanza alichokishikilia.
Lady Jaydee
970506_10151529866700025_289971427_n
Vuguvugu la Anaconda limemrudisha rasmi kwenye chart mwanadada huyu mkongwe. Licha ya kulianzisha vuguvugu hili kwa matusi, mashambulizi na madongo mazito dhidi ya wapinzani wake wakubwa, Clouds FM, Lady Jaydee alijikuta akiungwa mkono na watu wengi na kupandishwa juu kutoka chini alikokuwa amekaribia kupotea.
Uhai wake ulirejea rasmi baada ya show yake ya miaka 13 kwenye muziki kwa kufanya show iliyomuingiza mpunga wa kutosha. Mwaka huu amefanikiwa kuwa na hits mbili namba moja, Joto Hasira na Yahaya. Kwa wiki sita mfululizo, Yahaya imeendelea kushika nafasi ya kwanza kwenye Marimba Music Chart, MMC na bado haoneshi dalili za kupunguza kasi.
Hadi sasa, Lady Jaydee ndiye msanii wa kike anayepata mashavu zaidi kuliko mwingine yeyote.
Ommy Dimpoz
Ommy-Dimpoz-aktitoa-salamu-kwa-fans-wake.
Wengi hawajui ukweli huu, kwamba baada ya Diamond, huenda Ommy Dimpoz akawa msanii anayelipwa fedha nyingi zaidi kwa sasa. Tangu mwishoni mwa mwaka jana alipoachia single yake iliyompa tuzo, Me and You aliyomshirikisha Vanessa Mdee, Ommy amekuwa ni mtu wa show zisizokauka.
Mwaka huu aliongoza kwa kuwa na nominations nyingi zaidi kwenye KTMA na kuibuka na tuzo tatu. Kama ilivyo kwa Diamond, Ommy ni msanii anayechaji fedha nyingi zaidi kwa show sasa hivi kiasi kilichomfanya azikatae shilingi milioni 8 alizoombwa alipwe na kampuni ya Global Publishers kwenye tamasha la Matumaini.
Hivi karibuni aliandaa show yake mwenyewe nchini Burundi iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa, ameendelea kuwa mmoja wasanii kwenye show za Fiesta mwaka huu na hivi karibuni, akiwa na single mpya, Tupogo, ataanza ziara yake nchini Marekani.
AY
fd3e6f2a192211e3a5e422000aaa08f8_7
Kwa muda mrefu, AY ameendelea kuimarisha mizizi yake kimataifa na hadi sasa, hakuna msanii wa Tanzania mwenye mafanikio makubwa kimataifa kama yeye. Akiwa na tuzo ya CHOMVA 2012 mkononi aliyoipata kutokana na video ya wimbo wake, I don’t Wanna Be Alone, wiki iliyopita AY alikuwa msanii pekee wa Tanzania kutaja tena kuwania tuzo hizo zinazojulikana sasa hivi kama CHOAMVA katika vipengele viwili.
Mwaka huu ameachia ngoma mbili pekee, Jipe Shavu aliyomshirikisha Fid Q na Bila Kukunja Goti aliyoifanya na swahiba wake Mwana FA na kumshirikisha Mnaijeria, J-Martins. Hivi karibuni yeye na Mwana FA wameshoot video ya Bila Kukunja Goti nchini Afrika Kusini na hakuna shaka kuwa ikitoka itachezwa kwenye vituo vikubwa vya runinga.
Pamoja na jitihada hizo AY, imekuwa ngumu kwake kutajwa kwenye tuzo za KTMA hali iliyomfanya Mwana FA aandike: “Back to the drawing board,hii wimbo imeshinda huku,si ‘kill music awards’ waliigomea,kuwa haikuwa inafaa hata kuwa kwenye nominations zao. Ina maana viwango vyao ni vya juu hivyo?kuwa unaweza shinda channel O vya kwao ukawa hujavifikia?ama kubana kwao kwa kipuuzi kumeumbuliwa? I’m not mad..what my boy @AyTanzania won is much much bigger than ‘KILL music awards’..I’m just concerned…that was ALL.”
Mwana FA
IMG_1043 (800x534)
Mwaka huu Hamis Mwinjuma aliandika historia baada ya kufanya show ya hip hip kwenye ‘corporate audience. Ikipewa jina, The Finest, Mwana FA alisindikizwa na bendi kongwe ya Kilimanjaro aka Njenje kuangusha show iliyofanikiwa sana.
Uhusiano wake na Njenje ulizalisha wimbo wake Kama Zamani ambao tayari video yake imeendelea kufanya vizuri na pia kuchezwa Channel O. Mwaka huu Mwana FA alikuwa msanii wa tatu miongoni mwa wasanii wa Tanzania wanaoingiza fedha nyingi kwenye miito ya simu, nyuma ya Rose Mhando na Diamond kwa kuingiza shilingi milioni 18.
028d97ea158511e3bdf822000a1fa51c_7
d29014bc163a11e393af22000a9e05e8_7
Mafanikio yake mengine yana uhusiano wa moja kwa moja na yale ya AY kwa ushirikiano wao wa siku nyingi na hivi karibuni wote walienda nchini Kenya kutengeneza nyimbo mbili na producer mkongwe, Eric Musyoka wa Decimal Records.
Chege na Temba
Temba-na-Chege-wakifanya-makamuzi.
Ni ngumu kuyasema mafanikio ya Chege bila kumtaja Temba na vice versa. Kwa muda mrefu, wakali hawa wameendelea kuwa pamoja na hivi karibuni kwenye show za Fiesta wameendelea kutajwa kuwa wasanii wanaoshangiliwa zaidi kwa kufanya show nzuri kuliko wengine.
Nay wa Mitego
Nay-Wa-mitego.
Mwaka huu umekuwa mzuri kwa Nay wa Mitego hasa kwakuwa amekuwa akipiga show nyingi zinazomuingizia mkwanja mzuri. Nay wa Mitego amehit zaidi na Muziki Gani aliomshirikisha, Diamond Platnumz. Wimbo huo ulimsaidia kumfungulia zaidi milango ya neema rapper huyo controversial. Baada ya kuachia wimbo wake mpya, Salam Zao, Nay alirejea tena kwenye midomo ya watu, blogs, magazeti na kwenye vituo vya redio na TV kuhusiana na yale aliyoyasema kwenye wimbo huo. Lakini kama usemi usemavyo, promotion yoyote ile ni promotion nzuri, aina hiyo ya uimbaji imeendelea kumweka pazuri.
Ben Pol
16108fe3bd5c41aa34be321b5457b6e6
Ben alijikuta mahali pazuri zaidi baada ya mwaka huu baada ya kushinda kipengele cha mtunzi bora wa mashairi ya Bongo Flava kwenye KTMA. Na baada ya kuachia video yake ya Jikubali, Ben Pol ameendelea kupanda juu kwa spidi huku akiwa msanii anayetafutwa zaidi kwaajili ya chorus.
Stamina na Young Killer
page
Jana na Leo, imewaweka karibu zaidi rappers hawa japokuwa kila mmoja ana nyimbo zake zinazofanya vizuri. Mwaka huu Young Killer aliuingia na wimbo wake Dear Gambe ambao laiti kama angekuwa na umri juu ya miaka 18, angechukua tuzo kibao za KTMA. Wimbo wake mpya sasa ni Mrs Superstar ambao umezidi kupigia mstari uwezo wake kimashairi. Kwake Stamina naye, Wazo la Leo aliomshirikisha Fid Q na Mwambie Mwenzio aliomshirikisha Warda na Darassa zimemweka pazuri na kujikuta yeye na Young Killer wakiwepo kwenye show zote za Fiesta zinazoendelea.
Madee
Madee-alianza-kumsaka-aliye-mwaga-pombe-yake-Mbeya.
Single moja tu, Sio Mimi, imemuingizia Madee zaidi ya shilingi milioni 130, na kuthibitisha kuwa, hit moja tu inaweza kubadilisha maisha ya msanii. Hadi leo jina la Madee halikosekani kwenye show nyingi kubwa na huku akiwa miongoni mwa wasanii wanaonekana kupata shavu la kufanya show nyingi zaidi za Fiesta mwaka huu.

Post a Comment

Previous Post Next Post