Waziri Lukuvi kuanza ziara Mikoa ya Katavi, Rukwa na Mbeya

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge) Mhe. William V. Lukuvi (MB) kuanza ziara rasmi leo tarehe 16 hadi 19 Septemba, 2013 katika Mikoa ya Katavi, Rukwa na Mbeya.
Katika ziara hiyo Waziri Lukuvi anatarajiwa kutembelea baadhi ya vituo vya Ununuzi wa Mahindi kwa ajili ya kuhifadhiwa kwenye Maghala ya National Food Reserve Agency (NFRA), Maghala ya NFRA ya kuhifadhi chakula, atapokea taarifa ya Utekelezaji kuhusu Mradi wa Miundo Mbinu ya Masoko na Uongezaji wa Thamani (MIVARF) katika maeneo yanayotekeleza mradi huu.
Vilevile Mhe. Lukuvi atapokea Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi yote ya Maendeleo ikiwemo Miradi itokanayo na ahadi za Mhe. Rais na Miradi itokanayo na Ilani ya Chama Tawala pamoja na Miradi inayofadhiliwa na Taasisi mbalimbali Mkoani humo

Post a Comment

أحدث أقدم