Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe Amteua Brigedia Jenerali Mstaafu, Balozi Francis Mndolwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) amemteua Brigedia Jenerali Mstaafu, Balozi Francis Mndolwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo cha  Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

Balozi Mndolwa ameteuliwa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Wilson Masilingi ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi hivi karibuni. 

Brigedia Jenerali Mstaafu Mndolwa aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi kabla ya kustaafu utumishi wa umma.

Uteuzi wa Balozi Mndolwa unaanza mara moja.
Imetolewa na: 

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, 


DAR ES SALAAM
12 SEPTEMBA, 2013.

Post a Comment

أحدث أقدم