Habari ya kuondolewa kwa wimbo wa
Madee ‘Tema Mate’ kwenye kinyang’anyiro cha KTMAs bila shaka
zimewasikitisha wanafamilia wa Tip Top Connection na mashabiki
walioipendekeza kwa kura nyingi ngoma hiyo.
Kwa upande wa Madee amesema kuwa
BASATA wamechelewa katika kuchukua uamuzi huo kwa kuwa wimbo ulitoka
zamani na kushika nafasi ya kwanza kwenye chart nyingi za radio.
“Mimi nahisi walikuwa wamechelewa
ndio maana kila siku nalilia kwamba kuwe kuna chombo ambacho muziki wetu
tukishamaliza kuutengeneza tunapitisha pale then wanasikiliza kama
inafaaa kwenda hewani inafaa kama haifai tunaaambiwa mapema. Lakini
chombo hicho hakuna, kwa hiyo wanakuwa kama wanafake kwa sababu mwisho
wa siku wimbo unakuwa unasambaa na watu wanakuwa wameshaipenda.” Amesema
Madee.
Ameeleza kuwa kutokana na kuchelewa
huko watangazaji wa radio na Television ambao wanakuwa wanacheza wimbo
huo na kuuweka kwenye chart kama namba moja, pale unapozuiwa nao
wanaonekana kama hawana maadili bora.
Rapper huyo wa Manzese ameeleza kuwa
hafahamu hasa kwa nini wimbo huo umeonekana hauna maadili wakati yeye
alijua mara ya kwanza kuwa video ya wimbo huo ndiyo iliyokuwa imetajwa
kuwa kinyume na maadili.
Hata hivyo, Madee amesema tangu aanze
muziki miaka 14 iliyopita hajawahi kupata tuzo ya Kili hivyo haoni
hasara yoyote kwa kuondolewa kwenye kinyanyiro hicho.
“Nimeshazoea yaani haitoniaffect
chochote na wala haitakuwa na hasara yoyote kwenye muziki wangu, zaidi
tu ni kuwashukuru wale ambao walisapoti muziki wangu ukafika huko mpaka
watu wakakaa leo kuijadili, wamepoteza dakika zao kadhaa kuijadili kwa
hiyo ni kawaida mimi sioni kama nitaathirika na chochote.” Madee
ameongeza.
Tovuti ya Times Fm ilimtafuta kaimu
katibu mtendaji wa BASATA, Godfrey Mnengereza na kumuuliza mtazamo wake
na BASATA kuhusu alichokisema Madee.
“Nimependa sana maoni ya Madee, kumbe
tuko pamoja kwamba hazungumzii kwamba wimbo wake haukidhi hivyo vigezo.
Anazungumzia na anatoa ushauri kwa baraza kwamba tumechelewa kwa sababu
wimbo umepigwa mwaka mzima na kwamba tufanye censorship. Kwa sasa hivi
ni kweli ninakubali kabisa kwamba si sahihi sana wimbo uende hewani
ndipo tuanze kuzuia.” Amesema Godfrey Mnengereza.
“Kwa upande wa tuzo mchakato wake
ndio umeenza sasa na tunaangalia kazi zilizopita. Lakini nimeshukuru
sana kwa ushauri wake kwamba tuweze kufanya censorship, na ndiko
tunakoelekea kwamba katika suala zima la urasimishaji kazi yoyote ya
muziki wa audio inabidi ipite baraza, sasa ni kwamba tu ni kitu bado
kigeni. Lakini vile vile tunatakiwa tushirikiane na vyombo vya habari
kwamba wasiruhusu kazi ambazo zinamdhalilisha msanii mwenyewe, au zina
matusi ndani yake au zina lugha ya uchochezi.” Kaimu Katibu mtendaji wa
BASATA ameileza tovuti ya Times Fm.
Mbali na wimbo wa Madee ‘Tema Mate’,
nyimbo nyingine zilizoondolewa kwenye KTMAs kwa madai ya kukiuka maadili
ni Uzuri Wako ya Jux, na Nimevugwa ya Snura
إرسال تعليق