Baraza la Sanaa na Idara ya Uhamiaji wazungumzia biashara ya ngono inayofanywa na wasanii wanaotoka nje ya nchi

BARAZA La Sanaa Taifa (BASATA), limekiri kuwepo kwa baadhi ya wasanii wa nje kuja nchini kufanya shughuli za kisanii kutumia vibaya vibali vyao, kwa kujihusisha na masuala ya 'ngono' katika kumbi mbalimbali za starehe zinazojulikana kwa jina la 'Mujra Club'.
Hali hiyo imebainika baada ya Idara ya uhamiaji kubaini kuwa kuna baadhi ya maofisa wa idara hiyo kudaiwa kupokea rushwa ili kusaidia mtandao unawezesha kushamiri kwa biashara ya ngono zinazofanyika 'Mujra Club'.
Ambapo baadhi ya wasichana hao kutoka nchi za India, Nepal, Pakistan pamoja na Bangladesh kuja nchini kufanya kazi za sanaa kutumia vibaya vibali hivyo kwa kufanya biashara ya 'ngono' pamoja na biashara haramu ya binadamu.
Akizungumza ofisini kwake Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza alisema kuwa kurikuwepo na taarifa hizo kwa siku za nyuma ingawa hivi sasa hawajapokea taarifa zoote.
Mtendaji huyo alieleza kuwa hizo ni tuhuma ambazo zilishawahi kutokea kipindi cha nyuma, kilichohusisha kikundi cha wasichana wenye asili ya Asia ambapo walijifanya wasanii kuja nchini kufanya kazi za kisanaa.
Alieleza kuwa hali ilikuwa tofauti na maelezo yao kwani walikuja kubainika kuwa hawakuwa wasanii, bali walitumia jina la usanii kupata vibali na matokeo yake walitumia vibaya vibali hivyo kwa kujihusisha na masuala ya 'Ngono', katika baadhi ya kumbi za starehe.
Aliongezea kuwa kwa hivi sasa bado hawajapokea taarifa zozote, ingawa amewataka watu wanaojihusisha kuleta wasanii nchini kuwa makini, hivyo wakibaini kuna matumizi yoyote mabaya ya vibali hivyo vinavyotolewa watachukua sheria kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji.
Hivi karibuni Idara ya Uhamiaji kupitia msemaji wa Idara hiyo, Abbas Irovya alitoa taarifa ya kuwepo kwa tuhuma kwa baadhi ya wasanii wanaokuja nchini kutumia vibaya vibali vyao kwa kujihusisha na masuala ya ngono.

Post a Comment

Previous Post Next Post