Kufuatia
kuwepo kwa hoja mbalimbali za wajumbe wa Bunge maalum la katiba kuhusu
kukinzana kwa Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati wa uzinduzi
wa bunge hilo na rasimu ya katiba iliyowasilishwa na mwenyekiti wa tume
ya mabadiliko ya katiba jaji Joseph Warioba, mwenyekiti wa bunge maalum
Samwel Sitta ameridhia kujadiliwa kwa hotuba hizo.
Amesema baada ya kutolewa kwa hotuba hizo amekuwa akipokea maombi ya
Wajumbe mbalimbali wakishauri kutaka zijadiliwe na kupendekeza mjadala
huo ufanyike siku ya Jumatano wiki hii.
Kauli ya Mwenyekiti huyo imetokana na muongozo ulioombwa na mmoja wa
wajumbe wa Bunge hilo Julius Mtatiro aliyetaka mwenyekiti wa tume ya
mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Warioba aitwe bungeni kujibu baadhi ya
hoja zilizotolewa na Rais kikwete ambazo zinapingana na rasimu
iliyowasilishwa.
Namkariri Mtatiro akiuliza ‘kwa sababu Rais alikaribishwa tu kwa
heshima kwenye bunge hili kuja kufungua na sasa akaanza kujibu ile
hotuba, hatuoni kama kuna haja ya kujenga utaratibu wa kumleta tena mtoa
hoja ili na yeye aje kujenga hoja juu ya maswali aliyoeleza Rais?’
Kwenye sentensi nyingine mwenyekiti wa Bunge hili maalum la katiba
Samwel Sitta ameunda kamati 12 zitakazokuwa zikijadiliana kuhusu ibara
za katiba zitakazopangwa kwa ajili ya kuwasilishwa bungeni kwa mijadala
ya jumla.
إرسال تعليق