Lady Jaydee aanza ku-tease wimbo wake mpya unaokuja, unaitwa ‘NASIMAMA’.

Lady Jaydee pamoja na Machozi Band akitumbuizaMwanamuziki Judith Wambura aka Lady Jaydee ameanza kutease wimbo wake mpya unaokuja ikiwa ni ishara ya kuwa muda si mrefu anatarajia kuachia single mpya baada ya ‘Historia’.
Jide kupitia ukurasa wake wa Facebook wenye likes zaidi ya 250,000 amewaonjesha mashabiki wake sehemu ndogo ya wimbo huo unaoitwa NASIMAMA, lakini sio kwa njia ya sauti wala video bali ni mashahiri ya kiitikio cha wimbo huo.
“Chorus ya wimbo wangu mpya ambao haujatoka unaoitwa NASIMAMA: maneno haya hapa… kwa wale wanaopenda ku sing along muda utakapofika.
CHORUS: Aliepanga ni maanani, shida na riziki zangu
Aliezitupa gizani, shida na tabu zangu oooh x2
Rahisi eeeh?? beti zilizosalia nita post siku zijazo” Aliandika Jide

Post a Comment

أحدث أقدم