Ingawa Roma Mkatoliki anaishika Tanzania kwa nyimbo zake na
kueleweka sana kwenye masikio ya watu wengi hasa vijana, mama yake mzazi
sio shabiki wake mkubwa na anawakubali waimbaji wengine zaidi yake.
Rapper huyo toka Tanga ameeleza kupitia kipindi cha Bongo Dot Home
cha 100.5 Times Fm wakati anapiga story na Jabir Saleh, Moko Biashara na
Godzilla.
Roma amemtaja Linex kuwa kati ya wasanii watatu ambao mama yake mzazi
anawapenda zaidi lakini siku zote analalamikia uvaaji wake wa suruali.
“Bibi Mkubwa kwanza mimi anawasanii watatu ambao anawakubali sana.
Anapempenda Sunday Linex, anampenda Barnaba…huwa anasema ‘yaani Linex
mimi na mpenda sana sema mlegezo tu, hapo ndo ananivuruga hapo
anashindwaje kupandisha.” Ameeleza Roma Mkatoliki. “Nakwambia Linex
akiperform anatamani akimbie akabebe suruali aipandishe.” Aliongeza kwa
utani.
Mkali huyo wa ‘KKK’ amewataja wasanii ambao wanapendwa zaidi na mama
yake ukiacha Linex ambaye ndiye ‘favorite artist’ wake kuwa ni Barnaba,
Bushoke na Ben Pol.
Lakini inapokuja kwenye suala la kusikiliza rap za Rhymes Of Magic and Attraction (R.O.MA), bado mama hajazielewa.
“Mimi mother naona hanielewagi, naonaga hanielewagi. Labda nilete
mpunga ndo kidogo anacheka kwamba mwanangu unaimba vizuri lakini
naonaga kama sio big fan wangu. Kwa sababu mimi naweza kukaa home
nasikiliza mangoma, labda namsikiliza mwanangu Ben Pol anavyorindima
unaoma kabisa mama anafeel kabisa eeeh, lakini labda Mr. President
ikaanza pale ‘Ikulu’ unasikia eeeh hebu punguzeni sauti, nyimbo nyingine
zina kelele, unaona hapa kama mama kakaza daah.”
Msikilize hapa:
إرسال تعليق