NAIBU
WAZIRI WA FEDHA MH:MWIGULU LAMECK NCHEMBA ZIARANI NCHINI UFARANSA NA
UJERUMANI KUHUDHURIA MKUTANO WA ACP NA DEVELOPMENT COOPERATION FORUM
Naibu
Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Lameck Nchemba ameanza ziara yake ya Kikazi
Nchini Ufaransa kwa Muda wa Siku mbili (Tar.18 na 19/03/2014) atakapo
hudhuria Mkutano wa Umoja wa Nchi za Africa,Caribbean na Pacific.Mkutano
huo ni Miongoni mwa Mikutano ilinayofanyika Kila Mwaka ya Umoja
huo.Kwenye Mkutano huo Mh.Mwigulu Nchemba natarajia Kushiriki Mjadiliano
ya namna ya Kuzijengea Uwezo madhubuti Nchi zinazoendelea katika
Maswala ya Biashara na Uwekezaji.Pia watafanya tathimini ya Utekelezaji
wa Mikakati ya Maendeleo waliokuwa Wamejiwekea Mwaka 2013.
Baada ya Ufaransa,Mh.Mwigulu Nchemba
ataelekea Nchini Ujerumani kuhudhuria Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano
wa Maendeleo (Development Cooperation Forum),Mkutano utakao husisha Nchi
zilizoendelea,Zinazoendelea na Taasisi Kubwa za Kifedha na Maendeleo
Duniani.
Katika Mkutano huu wa Ujerumani,Washiriki watajadiliana namna Misaada inayotolewa inavyotumika Kwenye Shuguli zilizolengwa za Maendeleo na Vile Vile Utekelezaji wa ahadi za Utoaji wa Misaada kutoka Nchi zilizoendelea katika hali ya Uwazi.

Naibu Waziri wa Fedha atakuwepo Ujerumani kwa Muda wa Siku mbili(Tar.20 na 21/03/2014).
Mungu Ibariki Tanzania.
إرسال تعليق