Mtandao
wa kijamii wa , Twitter, unafungwa nchini Uturuki , saa chache baada ya
waziri mkuu , Recep Tayyip Erdogan, kuahidi kuuondoa .
Bwana
Erdogan — ambaye anakabiliwa na kashfa kubwa ya ufisadi aliwaambia
maelfu ya wafuasi wake katika mkutano wa uchaguzi kuwa hajali kuhusu
namna jamii ya kimataifa itakavyochukulia hatua yake .
Neelie Kroes, ambaye ni naibu rais wa tume ya muungano wa Ulaya amesema umamuzi wa kufungwa kwa mtandao huo ni wa kulaumiwa .
Serikali
ya Bwana Erdogan imekuwa ikilalamika kuwa mtandao wa Twitter ulipuuza
uamuzi wa mahakama ulioitaka viunganishi vya taarifa zake vinashukiwa
kurekodi mawasiliano yake binafsi.
CHANZO: BBCSWAHILI
Post a Comment