KOCHA Arsene Wenger leo amekabidhiwa tuzo ya dhahabu kwa kufikisha mechi 1,000 akiwa kazini Arsenal.
Mfaransa
huyo atafikisha mechi ya 1,000 kesho atakaposafiri na The Gunners hadi
Stamford Bridge kumenyana na Chelsea katika Ligi Kuu ya England mchana.
Kuheshimu
hilo, Mwenyekiti wa Arsenal, Sir Chips Keswick amemkabidhi Wenger tuzo
hiyo leo asubuhi katika viwanja vya mazoezi ya klabu mbele ya Waandishi
wa Habari.
Washika
Bunduki: Wenger akiwa na Mtendaji Mkuu, Ivan Gazidis (kushoto) na
Mwenyekiti Sir Chips Keswick (kulia) baada ya kupokea tuzo yake
Akizingatia
wa timu kufanya vizuri na kufanya vibaya akiwa kazini, Wenger aliyeipa
timu hiyo mataji matatu ya Ligi Kuu ya England na manne ya Kombe la FA,
alisema; "Kila
kipigo unachopata ni maumivu moyoni ambayo huwezi kusahau, na kila
ushindi ni wa kusahau kwa sababu unachukuliwa ni kawaida,".
Aliongeza; "Kumekuwa na msoto mkubwa katika mechi 1,000. Kitu ninachotaka wakati ujao wa furaha,"alisema.
Alipowasili: Wenger alikuwa hafahamiki wakati anatambulishwa Uwanja wa Highbury (sasa Emirates) Septemba mwaka 1996
Wakati
wa furaha: Wenger akiwa ameshika taji la ubingwa wa Ligi Kuu wakati
Nahodha, Tony Adams akiwa ameshika Kombe la FA baada ya Arsenal kushinda
mataji mawili msimu wa 1997-1998
Post a Comment