.
DROO
ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya imekalimika muda
mfupi uliopita ambapo Manchester United wameangukia mikononi mwa
mabingwa watetezi wa kombe hilo Bayern Munich.
Timu
pekee nyingine ya England iliyosalia UEFA, Chelsea yenyewe imepangiwa
mabingwa wa Ufaransa, Paris Saint-Germain baada ya chungu kuzungushwa
na nyota wa zamani wa Ureno Luis Figo.
FC
Barcelona imepangwa kuumana na timu iyocheza nayo ligi moja, Atletico
Madrid, wakati Real Madrid wataoneshana kazi dhidi ya wakali wengine wa
Bundesliga, Borussia Dortmund.
Mwari huyo!: Kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya likiwa limewekwa Nyon, Switzerland wakati wa droo mchana huu
Wamevurugwa: Wayne Rooney na Manchester United watautafuna mfupa wa Bayern Munich?
DROO YA ROBO FAINALI IMEMALIZIKA HIVI
Barcelona vs Atletico Madrid
Real Madrid vs Borussia Dortmund
Paris Saint-Germain vs Chelsea
Manchester United vs Bayern Munich
Mechi za kwanza zitachezwa mwezi wa nne tarehe 1 na 2, wakati mechi za marudiano zitapigwa mwezi wa nne tarehe 8 na 9.
David
Moyes alifuzu kwa juhudi kubwa baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi
ya Olympiacos dimba Old Trafford ambapo mechi ya kwanza nchini Ugiriki
alipigwa 2-0. Lakini sasa amepewa kazi nyingine ngumu zaidi kama
anataka kufuzu nusu fainali.
Moyes
ambaye bado yupo katika msongo wa mawaza kufuatia kipiga cha 3-0 kutoka
kwa Liverpool wiki iliyopita, atakutana na kocha wa zamani wa
Barcelona, Pep Guardiola ambaye sasa yupo Allianz Arena.
Bayern
ambao waliwatupa nje Man United mwaka 2010 walikuwa wa kwanza katika
kundi lao lililokuwa na klabu za Manchester City, CSKA Moscow na
Viktoria Plzen.
Amefurahi?
Samuel Eto’o na Chelsea yake wameliwatoa Galatasaray baada ya
kuwafumua mabao 2-0 uwanjani Stamford Bridge hatua ya 16.
Vijana wakubwa: Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo (kulia) na Gareth Bale wanatafuta kombe lingine
Mabingwa watetezi!: Bayern Munich walifuzu robo fainali baada ya kuwalowesha Arsenal
Hatari sana!: Zlatan na Paris Saint-Germain yake walifuzu baada ya kuwatoa Bayer Leverkusen
Usitusamehe: Lionel Messi na Barcelona yake waliwatungua Manchester City na kufuzu robo fainali
PICHA NA SPORTSMAIL
Post a Comment