Nazizi akanusha kuwa na uhusiano na producer Mtanzania Sappy wa Homeboyz

Rapper wa Necessary Noize Nazizi amekanusha habari za kuwa na mpenzi mpya ambaye ni producer wa Homeboyz Productions ya Kenya Mtanzania Kheri Sappy, baada ya kuachana na mume wake hivi karibuni.
sappy1 Nazizi akiwa na Sappy
Kwa mujibu wa Nairobi Wire, Nazizi amesema kwa sasa bado yupo single.
“Nina marafiki wengi wa kiume, tunapiga picha kila mahali, hivyo ndivyo uhusiano wangu na marafiki zangu ulivyo”. Aliiambia Nairobi News.
sappy4
Nazizi mwenye mtoto mmoja aliongeza kuwa hatashangaa kuona picha zingine zikitoka lakini akaendelea kusisitiza kuwa ana marafiki wengi wa kiume ambao yuko karibu nao.
“In fact, I won’t be surprised when more pictures come out. Like I said, I’m currently not seeing anyone, I just have many friends who are male and whom I am very close to.”
sappy3
Weekend iliyopita Sappy aliithibitishia Bongo5 kwa ushahidi wa picha pia kuwa yeye na Nazizi sasa ni wapenzi ambao wana mipango mikubwa juu ya uhusiano wao.
Aliongeza kuwa uhusiano wao ulianza kipindi cha Valentine ya mwaka huu Feb 14 na kuwa wanapendana kwa dhati.

Post a Comment

Previous Post Next Post