‘NI LAZIMA TURUDI UPYA - ROONEY:

>>ROONEY ATAKA KULIPA FADHILA KWA MASHABIKI!
>>WACHEZAJI WAKITOKA NJE BAADA KUFUNGWA, MASHABIKI OLD TRAFFORD WALIIMBA: ‘MARA 20 MAN UNITED!’ KUSAPOTI TIMU!
ROONEY_KIDOLE_JUUWayne Rooney amewasifia Mashabiki wa Manchester United kwa kusimama imara pamoja nao licha ya Jana kufungwa 3-0 na Liverpool.
Kwenye Mechi hiyo, Mashabiki wa Man United waliojazana Old Trafford walikuwa wakiimba mfululizo kwenye Mechi nzima licha ya kufungwa na baada Mechi kwisha, huku Wachezaji wakitoka nje ya Uwanja, Mashabiki hao waliwashangilia na kuimba Nyimbo murua ya kuvutia '20 times Man United' ikiwa ni Saluti kwa Timu yao kutwaa Ubingwa wa England mara 20.
Akiongea na MUTV, TV ya Man United, Rooney alieleza kuwa yeye na wenzake wana nia kubwa kulipa fadhila kwa Mashabiki kwa kuwasapoti kwa kuifunga Olympiakos Jumatano kwenye Mechi ya Marudiano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ambayo Man United wanahitajika kupindua kipigo cha 2-0 cha Mechi ya Kwanza ili kutinga Robo Fainali.
++++++++++++++++++++++++++++++++++
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
MARUDIANO
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi ya Kwanza]
[Saa za Bongo]
Jumatano Machi 19
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP [0-2]
++++++++++++++++++++++++++++++++++
Rooney ameeleza: “Inahuzunisha lakini lazima turudi upya kwani tuna Gemu kubwa Jumatano. Mashabiki walikuwa safi sana kwetu. Wachezaji wote tunashukuru kwa hilo. Ni lazima tuwalipe!”
Kipigo hicho kimewaacha Man United wakiwa Nafasi ya 7 kwenye Ligi na wapo Pointi 12 nyuma ya Nafasi ya 4 ambayo ndio ya mwisho ya kuweza kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao na alipohojiwa kuhusu hali hiyo na kama wataweza kutinga 4 Bora, Rooney alijibu: “Nani anajua? Ni ngumu. Lakini tutajisukuma kwani lolote linaweza kutokea kwenye Soka. Kama nafasi ipo, tutajaribu tu. Kama itawezeka ni sawa, kama haiwezekani sawa, lazima tusonge mbele! Kitu muhimu ni kujitayarisha kwa Jumatano!”

Post a Comment

أحدث أقدم