Refa Andre Marriner huenda akawekwa kando kwenye michezo ya
mwishoni mwa juma baada ya kufanya makosa yakutoa kadi nyekundu kwa
mchezaji wa kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya Arsenal na Chelsea ambapo
Chelsea ilishinda 6 bila.
Marriner alitoa Penalti wakati wa mchezo wa siku ya Jumamosi baada ya
Alex Oxlade-Chamberlain kushika mpira, lakini Kieran Gibbs alipewa kadi
nyekundu na kuondolewa kimakosa. Oxlade-Chamberlain alionekana
akimwambia Refa kuwa yeye ndiye aliyeshika mpira, hata hivyo uamuzi wa
awali ndio ulikua wa mwisho.
Hata hivyo baadaye Mariner alikiri na kuomba radhi kwa makosa
yaliyojitokeza, akikiri kufanya makosa kutomtambua aliyepaswa kuadhibiwa
katika mchezo huo. Chama cha waamuzi wa mchezo wa kulipwa kimesema
kuwa matukio ya kumwadhibu mchezaji kimamkosa ni nadra kutokea na mara
nyingi husababishwa na sababu mbalimbali za kiufundi
Source:BBC
إرسال تعليق