Ripoti ya miezi 6 ya alichoingiza kutokana na miito ya simu yamnyong’oza Ben Pol, ‘najitoa rasmi’

Ben Pol
Ben Pol hafurahii tena biashara ya miito ya simu (Ring Back Tone, RBT) kwakuwa ripoti ya miezi sita kutoka kwa moja makampuni yanayohusika na biashara hiyo nchini kumkatisha tamaa muimbaji huyo wa ‘Unanichora’.
Ripoti ya kipindi hicho iliyotolewa na kampuni hiyo, inaonesha kuwa ameingia shilingi 31,124 tu. “Mimi picha ninayoipata hapo naweza kusema kuna utapeli,” Ben Po ameiambia Bongo5.
Amesema ameshawahi kuishtaki kampuni nyingine tofauti inayohusika na biashara hiyo baada ya kupewa ripoti ya mapato isiyoridhisha na ndipo alipoufahamu ukweli. “Kwasababu na mtandao pia uliingia kwenye lile sakata na wenyewe wakatoa invoice ambayo walikuwa wanawalipa wale, ni tofauti na hizo ripoti wanazotoa hawa third part. Kwahiyo ni straight kama ni udhulumati,” amesema Ben.
“Mimi najitoa na kampuni zote labda kama mtu aseme ananunua copyright ya kumiliki huo wimbo jumla ambayo watashindwa kwakuwa itakuwa bei kubwa sana.”

Post a Comment

Previous Post Next Post