THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S
OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA
RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA
MRISHO KIKWETE
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za
Rambirambi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Hawa A. Ghasia kufuatia kifo cha Mkuu wa
Mkoa wa Mara, Mhe. John Gabriel Tuppa, aliyefariki leo tarehe 25 Machi, 2014
katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.
Pokea rambirambi zangu za
dhati na masikitiko makubwa kufuatia kifo cha
Mhe. John Gabriel Tuppa. Ni huzuni kubwa na pigo kwa Serikali na hasa kwa
Watendaji wenzake mkoani Mara ambao alikuwa akifanya nao kazi. Marehemu John Gabriel Tuppa amefariki leo
tarehe 25 Machi,2014 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.
Rais pia amemwomba Mhe.
Ghasia amfikishie salamu za pole kwa Mke wa Marehemu,Watoto na Familia ya Marehemu kwa
kuondokewa na kipenzi chao. Rais amesema, anaelewa machungu wanayoyapitia
katika kipindi hiki kigumu kwani wamepoteza nguzo imara waliyokuwa wakiitegemea
katika maisha yao.
“Hakika tumempoteza kiongozi
mchapakazi ambaye amekuwa akijituma na
kuwatumikia Wananchi wake hadi dakika za mwisho za uhai wake. Pengo aliloliacha Marehemu Tupa haliwezi
kuzibika kamwe lakini hatuna budi kumwombea kwa Mwenyezi Mungu kuipumzisha roho
ya Marehemu mahali pema peponi” Amina.
Taratibu na maandalizi ya
mazishi zinafanywa kwa ushirikiano wa Familia, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na
Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI.
Marehemu Tupa alizaliwa
tarehe 01 Januari, 1950 na katika enzi za uhai wake amewahi kuongoza Wilaya za Chunya, Mwanga, Bukoba, Muleba na Dodoma
kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mwaka 2011. Ameacha Mke na watoto
watano.
Mwisho!
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES
SALAAM.
25 Machi,2014
إرسال تعليق