Sista (mtawa) aliyeshiriki shindano la kuimba ‘The Voice Italy’ na kuimba wimbo wa Alicia Keys ‘No One’


Shangwe na vifijo vilitawala kupita kawaida katika ukumbi ambapo shindano la kuimba la ‘The Voice’ version ya Italy lilifanyika, baada ya sista wa kanisani alipoamua kushiriki na kuimba wimbo wa Alicia Keys ‘No One’ mwanzo mwisho kwa uwezo mkubwa, kitu ambacho kiliwashangaza watu wengi kama sio wote.
Mbali na uwezo mkubwa wa kuimba aliouonesha katika shindano hilo lililofanyika March 19, lakini pia sista huyo aitwaye Cristina Scuccia mwenye miaka 25 alithibitisha kuwa mtumbuizaji na mchezaji mzuri awapo jukwaani.
Majaji wote wanne walishindwa kuficha hisia zao baada ya kugundua aliyekuwa anaimba ni sista tena akiwa katika mavazi rasmi ya watawa.
Mmoja wa majaji alimtania sista huyo kwa kumwambia “Kama ningekukuta katika misa ningekuwa nahudhuria kanisani kila siku”.
Video ya mtawa huyo akiimba katika shindano hilo imeshatazamwa mara 18,692,043 mpaka sasa toka ipandishwe Youtube March 19.
Tazama video hapo juu.

Post a Comment

أحدث أقدم