SEHEMU
moja ya jukwaa katika Uwanja wa Allianz Arena itafungwa wakati wa
mchezo dhidi ya Manchester United na wenyeji Bayern Munich mwezi ujao.
UEFA
imechukua hatua hiyo kuelekea Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya,
baada ya mashabiki wa Bayern kuonyesha bango la matusi katika mchezo wa
16 Bora dhidi ya Arsenal.
Bango
hilo lilikuwa limeandikwa "Gay Gunners", yaani Arsenal mashoga- na
kuchorwa kikatuni cha kiungo Mesut Ozil mbele ya klabu saini ya klabu
hiyo.
Utata: Mashabiki wa Bayern Munich wakionyesha bango la matusi kabla ya mechi na Arsenal
Adhabu: UEFA imeamua Arjen Robben na wenzake watacheza eneo moja la Uwanja likiwa tupu
Siti za gharama: Eneo namba 124 - lililozungushiwa wino mwekundu litakuwa wazi katika mechi na Manchester United
إرسال تعليق