Mji mkuu wa Burundi, Bujumbura
umekua na sifa ya kuwa na wakaazi wengi wanao fanya mazoezi ya mwili na
hasa mwishoni mwa wiki ambapo barabara zote hujaa makundi ya watu
wanaotembea au kukimbia.
Lakini kwa sasa yote hayo hayatofanyika bila
kupata ruhsa maalum kutoka manispaa ya jiji. Watu wengi wanaopenda
kufanya mazoez wanalalamika kuwa uhuru wao umekandamizwa.Meya amesema baadhi ya vyama au mashirika ya kisiasa yanatumia fursa ya kujikusanya kwenye michezo na mazoezi ya pamoja ili kuandaa maandamano au kuchochea ghasia na vurugu kwenye barabara mbali mbali kwa ukiukwaji sheria.
Ni marufuku watu kufanya mazoezi ya watu wengi barabarani badala yake imeruhusiwa kufanya mazoezi hayo katika maeneo maalum yanayoruhusiwa kufanyia michezo na mazoezi.
Katika taarifa hiyo Meya Said Juma amevitaja viwanja karibu tisa vya soka mjini Bujumbura kama maeneo yanayo ruhusiwa watu kufanya mazoezi wakiwa pamoja au kwa wingi.
Amri hii imetolewa baada ya purukushani iliyojitokeza mapema mwezi huu baina ya chama cha upinzani cha MSD na polisi ambapo zaidi ya wafuasi 50 wamefungwa jela maisha.
إرسال تعليق