
Wiki
iliyopita, mtu mmoja mwenye uraia wa Ghana kwa jina Boubacar Traore
(42), alikamatwa na kilo 3.5 za heroin zenye dhamani ya dola za
Kimarekani milioni 3 mara tuu baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege
wa kimataifa wa JFK, jijini New York, Marekani. Aliwasili uwajani hapo kwa ndege ya British Airways ikitokea London alikounganisha ndege.
Taarifa
zilizowasilishwa mahakamani zinaonyesha kuwa Traone alianzia safari
yake Tanzania lakini haijaelezwa alipitia JNIA au KIA. Hata hivyo, jana
Rais Kikwete alisema kuwa kuwa dawa za kulevya zinazidi kupita katika
viwanja vya ndege vya JNIA na KIA na kuwa hali hii inazidi kuchafua
heshima na jina la Tanzania.
Maafisa uwanjani
hapo (JFK) walishtukia begi moja (Samsonite roller bag) ambalo lilikuwa
limekaa kama halina mwenyewe vile. Baada ya kulichunguza walikuta kuwa
mmiliki wake alikuwa ni Traone ambaye ni baba wa watoto saba anayemiliki
grocery nchini Ghana. Baada ya begi hilo kupekuliwa maafisa hao
walikuta kilo 3.5 za heroin zilizokuwa zimefichwa kwenye begi hilo kama
linavyoonekana kwenye picha hapo chini.

Baada
ya kukamatwa Traore alikiri kosa lake la kushiriki katika kujaribu
kuingiza dawa hizo za kulevya Marekani na kukubali kushirikiana na
polisi ili kumkamata mshiriki mwingine. Baada ya kupiga simu kadhaa,
Traore alikubaliana kwenye simu kukutana na mtu mwingine kwa jina
Francis Abankwa (50) ambaye ni devera wa moja ya mabasi ya MTA
(Metropolitan Transportation Authority).
Abankwa alikuwa amepanga
kuchukua mzigo mida ya saa kumi jioni lakini alimwambia Traore asubiri
kidogo mpaka round ya mwisho kwa sababu basi lilikuwa limejaa abiria
wengi. Hivyo, walikubaliana kukutana saa 6.51 za jioni kwa saa za New
York katika kituo cha basi cha Grand Concourse and East Tremont
kilichopo Bronx, jijini New York. Wakati huo, Abankwa alikuwa bado hajui
kuwa Traore alikuwa tayari ameshakamatwa na dawa hizo. Pia hakujua kuwa
alikuwa amekubali kushirikiana na Homeland Security kumkamata na yeye
pia.
Baada ya Abankwa kuwasili katika kituo cha basi cha Grand
Concourse and East Tremon na basi lake, Traone alipanda kwenye basi hilo
akiwa na begi lililokuwa na dawa hizo za kulevya. Baada ya kupanda
basi, Abankwa aliendesha basi lake huku wakijadiliana juu ya dili lao la
dawa za kulevya. Mazungumzo yao yote yalikuwa yanarekodiwa na kifaa
ambacho Traore alivalishwa na polisi.

Pia
kwenye basi hilo kulikuwa na maafisa wawili waliokuwa wamevaa nguo za
kiraia na walipanda basi mapema kabisa kutokea huko lilipoanzia na
kujifanya kama abiria wa kawaida. Maafisa hao walishuka kituo cha pili
kabla y kufikia kituo cha mwisho. Baada ya basi kufika kituo cha mwisho,
abiria wote waliobakia walishuka ispokuwa Traore aliyebakia kwenye basi
na kurudi na dereva Abankwa hadi kwenye depot ya mabasi ya MTA
(Kingsbridge Depot) iliyopo Inwood.

Baada
ya kuliacha basi pale, walielekelea kwenye gari ya Abankwa na ndipo
polisi wapowazunguka na kumkamata Abankwa ambaye wakati huo alikuwa na
lile begi mikononi mwake. Abankwa ambaye yupo katika kituo cha mahabusu
cha Metropolitan kilichopo Brooklyn amefikishwa mahakami na kushtakiwa.
Traore nae ameshtakiwa lakini kwa mujibu wa rekodi za kimahakama amepewa
dhamana kwa bond ya dola 100,000.
Abankwa amefanya kazi MTA
miaka nane na mwaka 2012 alilipwa dola za Kimarekani 102,000 kama
mshahara pamoja na marupurupu mengine. Mwezi February mwaka huu
alishtakiwa kwa fraud baada ya kuchukua Medicaid benefits kwa ajili ya
mke na mtoto wake.
إرسال تعليق