Leo nitaendelea kwa kujadili madhara ya tatizo hili:
Madhara ya Tatizo la kutokwa na uchafu katika via vya uzazi (Vaginal discharge):-
Ugumba: Hii hutokea pale mashambulizi/maambukizi yanapofika kwenye mirija na kuleta uvimbe ambao huziba au kusababisha kutengenezwa kwa maji machafu mazito ambayo nayo huziba mirija na huua mimba kila inapotungwa.

Mwanamke kunuka/kutoa harufu mbaya wakati wote hata kama ameoga na
kuvaa vizuri: Huwa hali mbaya zaidi wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
Jambo hili husababisha mwanamke kuwa na aibu na kujitenga, kutengwa,
kujiona hana thamani na unyonge.
Kupata maambukizi katika njia ya mkojo yaani U.T.I: Hii ni kwa sababu
njia ya uzazi na ile ya mkojo zimekaribiana sana sehemu zinapoanzia
kwenye via vya uzazi vya mwanamke. Tatizo hili la uchafu ukeni
lisipotibiwa kwa uhahika na kuisha huchangia maambukizi katika njia ya
mkojo kuwa sugu na yanayojirudiarudia kwa mwanamke.
Maumivu wakati wa kutoa haja ndogo, kwenda haja ndogo mara kwa mara,
maumivu ya mgongo na kiuno na kutoa haja ndogo yenye rangi ya njano au
kijivu ni baadhi ya dalili za U.T.I
Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi/ uterus
Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi/ uterus
Mashambulizi haya kwenye mirija hudhoofisha viumbe wanaoitwa cilia
ambao wanamaumbile kama vijinyoya ambao wapo kwenye kuta za mirija ya
uzazi wakiwa na kazi kubwa ya kusukuma yai la uzazi kupita bila tabu
kuelekea kwenye mji wa mimba na hivyo yai halitofika kwenye mji wa mimba
na mimba itatunga.
Kwenye mrija wa uzazi na kukua hapo, kitu ambacho humlazimu mwanamke
kufanyiwa upasuaji kuondoa mrija ulioathirika na hivyo kubakiwa na mrija
mmoja.
إرسال تعليق