Stori: WAANDISHI WETU
KUNA madai mazito kwamba, yule
bilionea kijana anayemiliki kampuni ya uuzaji na usambazaji wa vifaa
vya nyumbani ya Home Shopping Centre ya Kariakoo jijini Dar es Salaam,
Said Saad Mohamed amehama Bongo baada ya lile tukio la kikatili la
kumwagiwa tindikali lililotokea mwaka jana maeneo ya Msasani, Dar.Habari
za uhakika kutoka chanzo makini ambacho pia kipo karibu na familia hiyo
ya kitajiri zinasema baada ya kukamilika kwa matibabu yake yaliyoanzia
nchini Afrika Kusini na baadaye Ujerumani na kupona, mfanyabiashara huyo
aliamua kuhamishia maskani yake kwenye Jiji la Dubai ambao ni mji mkuu
wa Muungano wa Nchi za Kiarabu (United Arab Emirates).Kule inasemekana bilionea huyo licha ya kuwa na biashara anamiliki nyumba.KISIKIE CHANZO CHETU“Said
hakai tena hapa Bongo, amehama yeye na familia yake, hivi sasa anaishi
Dubai. Unajua anaogopa kuendelea kuishi hapa baada ya lile tukio, ameona
anaweza kuuawa maana hajui nani ni adui nani rafiki, huwa anakuja mara
mojamoja, anakaa siku mbili tatu anaondoka zake,” kilisema chanzo hicho.NI UAMUZI WA FAMILIAInadaiwa
kuwa baada ya kutibiwa Afrika Kusini na kisha Ujerumani ambako
alifanyiwa upasuaji wa mafanikio wa macho yaliyokuwa yameathiriwa na
tindikali hiyo, familia ilikaa chini na kuamua kwamba ndugu yao asikae
tena Tanzania.“Kama suala ni biashara, hata Dubai ana biashara,
tena kubwa tu, sasa kwa nini asikae huko ambako ni salama kuliko hapa?
Kule ana nyumba nzuri na maisha ni mazuri, jamaa hawezi tena kurudi na
kuishi hapa, kimsingi amehama kimoja,” kilisema chanzo hicho.Jitihada
za kumpata bilionea huyo kupitia namba zake za simu za siku za nyuma
zilishindikana, kwani zote hazikuwa hewani, lakini mtu mmoja wa karibu
na familia hiyo maarufu zaidi Kariakoo, alithibitisha kuhama kwa
mfanyabiashara huyo, Mtanzania mwenye asili ya Yemen.KUMPATA MSEMAJI WA FAMILIA NI KAZI KUBWAUchunguzi
zaidi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, usiri umetawala kwenye
familia ya bilionea huyo ambapo kumpata msemaji imekuwa kazi kubwa.“Unajua
yaliyotokea ndiyo yametoa fundisho, huwezi kumpata mtu akasema chochote
kuhusu Said kwani kila mtu anaogopa, maana unaweza kusema huyu ni
rafiki kumbe ni adui mkubwa,” kilisema chanzo.MTUHUMIWA BADO KUKAMATWAKwa
mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Kinondoni, Dar es Salaam, ACP
Camillius Wambura alisema juzi kwamba mpaka sasa hawajafanikiwa kumpata
mtuhumiwa.“Kusema kweli sina taarifa kama kuna mtu aliyekwishakamatwa kuhusiana na kummwagia tindikali huyo bwana,” alisema Wambura.TUJIKUMBUSHESaid
alimwagiwa tindikali Julai 19, mwaka huu, mishale ya saa 2 usiku akiwa
kwenye moja ya maduka yake yaliyopo kwenye jengo analodaiwa kulimiliki
la Msasani Mall jijini Dar es Salaam.Ilielezwa kuwa baada ya
kumwagiwa tindikali alikimbizwa kwenye Hospitali ya Ami Wellness Centre
iliyopo Masaki, Dar lakini ndani ya kipindi kisichozidi dakika 60
alichukuliwa na kupandishwa ndege kupelekwa nchini Afrika Kusini.“Sehemu
ya usoni kushuka kifuani upande wa kulia na mkono wenyewe wa kulia
ndiyo maeneo katika mwili wa ndugu yetu yaliyoathirika zaidi na
tindikali,” alisema ndugu huyo wa ndani kabisa kwa sharti la kutotajwa
jina, akaongeza:“Jicho la kulia lenyewe lilipata athari kidogo,
kwani inaonekana wakati mmwagaji akifanya kile kitendo, yeye alifumba
macho kwa hiyo tindikali haikuingia ndani ya jicho.“Ila kwa vile
tindikali ilimwagika kwa wingi juu kwenye jicho la kulia na kutokana na
ukali wa tindikali aliyomwagiwa, imesababisha kutengenezwa kwa mtoto wa
jicho kwa hiyo hawezi kuona mbali.“Uamuzi wa kumpeleka
Ujerumani ulifikiwa baada ya kujiridhisha kwamba kule kuna wataalamu
kuliko Afrika Kusini. Oparesheni ya uso kubadili ngozi iliyoathirika,
vilevile kufanya upasuaji wa jicho na kuliweka sawa ni mambo ambayo
tulijiridhisha yanawezekana Ujerumani.”NYUMBANI KWAKE KARIAKOOJuzi,
Uwazi lilifunga safari hadi kwenye nyumba ya bilionea huyo, Kariakoo
lakini hakukuwa na ushirikiano wowote kutoka kwa mtu aliyedai ni mlinzi
wa nyumba hiyo.
Bilione huyo wakati akiwa katika matibabu baada ya kumwagiwa tindikali .
GPL
إرسال تعليق