KATIBA ya Wekundu wa msimbazi
Simba sc imekamilika baada ya kufanyiwa marekebisho na kukabidhiwa kwa
uongozi wa klabu hiyo chini ya mwenyekiti Ismail Aden Rage.
Katibu mkuu wa Simba sc, Ezekiel
Kamwaga amezungumza na waandishi wa habari leo hii na kueleza kuwa
tayari wameshakabidhiwa katiba yao kutoka serikalini na kinachofuata na
kuanza kwa mchakato wa uchaguzi .
Awali uchaguzi wa Simba ulitakiwa kufanyika wiki iliyopita, lakini kutokamilika kwa katiba kulikwamisha mchakato mzima.
Kamwaga alisema baada ya zoezi la
katiba kukamilika, kesho wanatarajia kukutana na kamati ya uchaguzi
chini ya mwenyikiti wake, Mwanasheria Dkt. Damas Ndumbaro ili kupanga
mchakato mzima.
Katibu huyo aliongeza kuwa baada
ya kamati kukutana, taratibu zote zitawekwa wazi na wenye nia ya
kugombea wataanza rasmi mchakato.
إرسال تعليق