Afisa Elimu Msingi wilaya Sengerema Bw. Juma Mwajombe akikadhiwa madawati.
Na Daniel makaka, Sengerema.
WALIMU
wakuu shule za msingi katika kata ya Bupandwa wilaya ya Sengerema mkoa
wa Mwanza wameombwa kutumia vyema madawati yaliyotolewa na uongozi wa
msitu wa Buhindi kwa lengo la kusaidia kutatua tatizo la madawati
katika shule hizo.
Hayo
yamesemwa na Afisa Elimu ya msingi wilaya ya Sengerema Bw Juma
Mwajombe katika sherehe za kukabidhiwa madawati hayo iliyofanyika
katika sherehe za Mei Mosi katika kata ya Bupandwa ambapo uongozi wa
msitu wa Buhindi ulikabidhi madawati 80 katika kata hiyo ambapo
yatagawiwa katika shule zote za kata hiyo .
Diwani wa kata ya Bupandwa Bw. Masumbuko Bupamba akitoa shukurani baaada ya kukabidhiwa madawati.
Akikabidhi
madawati hayo Meneja Msaidizi wa Msitu huo Bw Ernesti Madatta amesema
kuwa msitu wa Buhindi umekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii hiyo na
itaendelea kutoa misaada katika shule hizo ili kuleta usawa kwa kuwa
jamii hiyo inasaidia kulinda raslimali za msitu huo.
“madwati
haya yamegharimu zaidi ya shilingi za kitanzania milioni tatu fedha
taslimu na tutaendelea kutoa msaada kwenye jamii zinazotuzunguka,’
amesema Madatta.
Meneja msaidizi msitu Buhindi Bw. ERNEST MADATA.
Bw,
Madata aliongeza kuwa sambamba na kukabidhi madawati hayo pia msitu
huo unajenga kituo cha afya katika kata hiyo pia jengo la mama na
mtoto katika zahanati ya Bupandwa ambapo kila moja itagharimu shilingi
milioni sabini pia amewataka wananchi wa kata hiyo kushirikiana vema na
msitu huo kuleta ushirikiano wa dhati miongoni mwao.
Kwa
upande wake Diwani wa kata hiyo Bw Masumbuko Bupamba amemshukuru meneja
huyo jinsi wanavyosaidia jamii hiyo na amewaomba waendelee na juhudi
hizo za kusaidia jamii.
Msitu wa Buhindi.
إرسال تعليق