MCHUNGAJI wa Kanisa la KKKT, John
Solomoni, ameshangazwa na kitendo cha idadi ndogo ya wasanii kujitokeza
katika kununua mashamba ya bei rahisi yanayotolewa na Shirikisho la
wasanii Tanzania(SHIWATA( yaliyopo Kijiji cha Ngarambe Wilayani
Mkuranga.
Solomoni ambaye pia ni Katibu wa
kamati ya amani ya viongozi wa Dini mkoa wa Dar es Salaam,aliyasema
hayo juzi katika hafla ya kuoneshwa mashamba kwa wasanii hao iliyoendana
sambamba na maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema kitendo kilichofanywa
nawasanii inaonesha ni jinsi gani bado haewajaanza kujitambua katika
kutengenezamaisha yao ya mbeleni.
Alisema kiasi cha shilingi 200,000 kinachotozwa kwa ajili ya
msanii kupata ekari moja na nusu ni kidogo sana ukilinganisha na thamani
ya ardhi ilivyo sasa lakini anawashangaa kwa nini wasanii wameshindwa
kujitokeza kama ilivyotarajiwa.
“Hapa nimeambiwa shirikisho lina
wasanii zaidi ya 8000 wakiwemo wasanii wakubwa wenye majina lakini kwa
nini ni 95 tu ndio wanunue mashamba hii ni aibu na kushindwa kujitambua
nyie ni kina nani mbele ya jamii,”alisema Mchungaji Solomon.
.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkuranga,Saada Mwaruka,
alisema kama Wilaya watawapa ushirikiano wa hali na mali wasanii
waliochukua mashamba hayo ikiwemo kuwakopesha pembejeo za kilimo.
Mwaruka alisema wanataka waone eneo hilo linakuwa shamba
darasa la kuigiwa mfano jambo litakalowaamsha vijana wa Mkuranga nao
kujishughulisha na kilimo na kuona kilimo sio kazi ya waliokosa kazi
bali ni moja ya njia za kuwainua kiuchumi.
Naye Mwenyekiti wa Shiwata,
Cassim Taalib, alisema wameamua kubuni mbinu hiyo ili kuwaondoa wasanii
wa nchi hii katika umasikini.
Taalib alisema katika mashamba
hayo kuna jumla ya ekari 500 kwa ajili ya kulima huku awali walitangulia
kagawa eneo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba robo ekari kwa kila msanii
lililopo maeneo ya Mwanzega huko huko Wilayani Mkuranga ili nao waweze
kumiliki nyumba.
Alisema utaratibu huo ndio
ulitumiwa na Mwalimu Nyerere wakati wa kuhamasisha vijiji vya Ujamaa
ambako mpaka leo watu wameona matunda yake.
إرسال تعليق