Ni
wiki zinahesabika toka staa wa bongofleva Nay wa Mitego apate namba
mpya ya gari lake inayoendana na ile ambayo amekua akiitaja kwenye
nyimbo zake na kwenye page zake za mitandao ya kijamii. #966
Stori
nyingine ya leo ni kutoka kwa staa mwingine wa bongofleva ambae kila
anaefatilia huu muziki hapa bongo anamfahamu, ni yuleyule ambae amevunja
rekodi ya kuwa staa pekee wa Tanzania alieandikwa sana kwenye mitandao
ya kijamii na magazetini kwa miaka miwili mfululizo.
Ni
Diamond Platnumz ambae kwenye birthday yake hivi karibuni management
yake ilimzawadia gari aina ya BMW X 5 ambapo inaaminika amechukua namba
hizi kwa ajili ya mkoko wake aliozawadiwa……….. atakua msanii wa kwanza
kuweka jina lake badala ya namba kwenye gari.
Utaratibu
wa kuweka majina badala ya namba umeanza kutumika kihalali nchini
Tanzania ambapo watu mbalimbali wasio maarufu walishaanza kujiwekea
miezi kadhaa iliyopita ambapo ada yake ni milioni tano kwa miaka mitatu.
Mpango
wa mastaa kuweka majina kwenye magari yao badala ya namba tulizozizoea
umekua ukitumika kwenye nchi mbalimbali duniani ambapo kwa Afrika
Mashariki Uganda ndio inaongoza kwa kuwa na mastaa wengi waliotundika
majina kwenye mikoko yao.
Gari alilozawadiwa Diamond kwenye birthday yake.
إرسال تعليق