Usiku wa kuamkia leo ulikuwa ni
usiku wa bara la Afrika huku timu kadhaa zikijitupa uwanjani kutafuta
tiketi ya kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika yatakayofanyika
mwakani huko nchini Moroko.
Tunisia walikuwa wenyeji kucheza dhidi ya Senegal, hadi kipyenga cha mwisho Tunisia ikaibanjua Senegal bao 1-0.
Nao
mabingwa wa kihistoria Misri walimenyana na Botswana, hadi mwisho wa
mchezo huo wenyeji Misri wakaibuka kidedea kwa kuwaangamiza wageni wao
bao 2-0.
Mashabiki wa Ivory Coast walilazimika kulala mapema baada
ya timu yao kustushwa na D.R Congo kwa kupokea kichapo cha nyumbani cha
mabao 4-3.
Katika mechi zingine Cameroon iliiadhibu Sierra Leone
kwa jumla ya goli 2-0, Togo wakafanikiwa kuiburuza Uganda kwa bao 1 bila
majibu,
Zambia nao wakaifurusha Niger kwa jumla ya magoli 3-0
huku mabingwa watetezi Nigeria wakarejesha matumaini ya kufuzu baada ya
kuibanjua Sudani kwa jumla ya mabao 3-1. Nayo Ghana ikaizabua
Guinea kwa ushindi wa goli 3-1, huku Angola wakiiangamiza Lesotho kwa kipigo cha mabao 4 kwa mshanago.
Katika viwanja vingine Cape Verde wakaibomoa Mozambique bao 1-0, Mali ikachezea kichapo cha mabao 2-3 kutoka kwa Ethiopia. Nayo
Algeria
ikaikalisha Malawi mabao 3 bila majibu, huku Gabon ikitoshana nguvu na
Burkina Faso kwa sare ya 1-1 na Bafana bafana ikajiweka katika hatari ya
kufuzu kwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Congo.
إرسال تعليق