Aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime akifikishwa mahakamani wakati wa hatua za awali za kesi hiyo. ------------------------ |
Na Mwene Said wa Globu ya Jamii
MAHAKAMA Kuu
Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imefuta mwenendo wa kesi ya mauaji
iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini dhidi
aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime na wenzake 11,
wanaohusishwa na kuporomoka kwa jingo la ghorofa 16 katika mtaa wa
Indira Gandh na kuua watu 27 badala yake wafunguliwe mashitaka ya kuua
bila kukusudia.
Akisoma uamuzi
huo,Jaji Salvatory Bongole Ijumaa iliyopita baada ya kukubaliana na hoja
zilizowasilishwa mbele yake na mawakili wa
upande wa utetezi kuwa na mashiko ya kisheria. Jaji Bongole aliamuru washtakiwa kuendea kushitakiwa kwa makosa ya zamani ya kuua bila kukusudia na siyo makosa ya mauaji.
upande wa utetezi kuwa na mashiko ya kisheria. Jaji Bongole aliamuru washtakiwa kuendea kushitakiwa kwa makosa ya zamani ya kuua bila kukusudia na siyo makosa ya mauaji.
Alisema washtakiwa
wanastahili kuendelea kuwa nje kwa dhamana zao kama livyokuwa kabla
upande wa Jamhuri kubadilisha hati ya mashitaka yao Marchi 12, mwaka huu
kutoka mauaji ya bila kukusudia na kuwa kesi ya mauaji ya kukusudia.
Jengo lililoporomoka Marchi 29, mwaka 2013 katika mtaa wa Indira Gandhi ulioko katika wilaya ya Ilala, jijijini Dar es salaam na kuua watu 27. |
Jaji alitupilia hoja
za upande wa Jamhuri ulikuwa ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu,
Bernard Kongola kuwa hati ya mashitaka ya mauaji ya kukusudia
iliyowasilishwa mahakamani ilikuwa sahihi na inajitosheleza kuwawezesha
washitakiwa kupanga utetezi wao. Katika uamuzi wake uliopokelewa kwa
shangwe na washitakiwa na ndugu zao waliokuwa wamefurika katika viunga
vya Mahakama Kuu, Jaji Bongole alisema kuwa kitendo cha kubadilisha
mashitaka kutoka mauaji ya bila kukusudia hadi mauaji ya kukusudia
kulifanywa kwa nia mbaya na upande wa Jamhuri.
Alieleza kuwa upande
wa mashitaka ulikuwa na nia ya kuwafanya washtakiwa wabaki rumande na
hii ilidhihilishwa tangu awali pale walipofikishwa kwa mara ya kwanza
kwa kosa la mauaji ya bila kukusudia na upande wa mashitaka ukapinga
dhamana.
Mara baada ya
Mahakama ya Kisutu kuwapa washtakiwa dhamana upande wa Jamhuri ulikata
rufaa kupinga dhamana hiyo. Hata hivyo, Jaji Bongole alifafanua kuwa
upande wa Jamhuri uliachana na rufaa hiyo mara baada ya mwaka mmoja
kupita uliwasilisha Mahakama ya Kisutu maombi ya kubadilisha hati ya
mashitaka ya mauaji ya kukusudia.
“Mabadiliko haya
hayakufanywa kwa nia njema bali yalilenga kuwanyima haki washtakiwa…
Vitendo vya makusudi vya namna hii havikubaliki na vinapaswa kukoma mara
moja,” alisisitiza jaji huyo wakati akisoma uamuzi wa kuwabadilishia
washtakiwa hao hati ya mashitaka.
Mbali na Fuime,
washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Razah Ladha (68), Goodluck Mbaga
(35), Wilboard Mugyabuso (42), Mohamed Abdulkari (61), Charles Ogare
(48), Zonazea Oushoudada (60), Vedasto Richale (59), Michael Hemed (59),
Albert Munuo (56), Joseph Ringo (43) na Ibrahim Mohamed.
Katika kesi ya
msingi, upande wa Jamhuri unadai kuwa Marchi 29, mwaka 2013 katika mtaa
wa Indira Gandhi ulioko katika wilaya ya Ilala, washtakiwa hao waliwaua
watu 27.
Katika tukio hilo
watu 27 walipoteza maisha wakiwemo Yusuph Khari, Kulwa Alfan, Hamada
Musa, Kessy Manjapa, Hamis Mkomwa, Boniface Bernard, Suhail Karim,
Salman Akbar, Selemani Haji, Selemani Mtego, Sikudhani Mohamed, Ahmed
Milambo na Salum Mapunda.
Wengine ni Selemani
Mnyamani, John Majewa, Mussa Mnyamani, Devid Herman, William Joakim,
Abdulrahaman Mwiha, Emmanuel Christian, Mmanyi Ngadula, Adivai Desiki,
Emmanuel Wahai, Augustino Chuma, Gabriel Godwin Kamwela, Philipo
Kusimula, Betod Mwananengule na Zahda Abbas
Post a Comment