HABARI NJEMA KWA ARSENAL …GIROUD KUREJEA UWANJANI MAPEMA KULIKO ILIVYOTARAJIWA



OLIVER Giroud anaweza kurejea uwanjani mapema zaidi kuliko ilivyotarajiwa – na atakuwa sambamba na Danny Welbeck kuunda safu kali ya ushambuliaji Arsenal.

Bosi wa washika bunduki, Arsene Wenger amefichua kuwa Giroud anaweza akarejea mapema kabla ya mwakani baada ya upasuaji wa mguu wake ulioumia kufanyika kwa mafanikio.


“Giroud anaendelea vizuri sana”, Wenger aliiambia beIN Sports na kuongeza: “Naamini yuko mbele zaidi ya tarehe iliyotarajiwa, operesheni iimekwenda vizuri.

 “Welbeck na Giroud wanaweza kucheza pamoja kama washambuliaji wa kati au hata pembeni.

“Alipokuwa Manchester United, Welbeck aliweza kucheza kando ya Rooney na Van Persie na bado akafanya vizuri.”

Pichani ni namna Giroud anavyoendelea vizuri

Post a Comment

Previous Post Next Post